Friday, September 16, 2016

TBL Mwanza yashika nafasi ya pili kwa ubora barani Afrika

tuz1
Richmond Raymond akipokewa na  baadhi ya wafanyakazi wa TBL Mwanza baada ya kuwasili na tuzo za ushindi akitokea nchini Afrika ya Kusini
tuz2
Msafara wa kutoka uwanja wa ndege kupokea cheti cha tuzo
tuz3
Baadhi ya wafanyakazi katika picha ya pamoja muda mfupi baada ya kupokea tuzo ambayo kiwanda kimetunukiwa

tuz4
Baadhi ya wafanyakazi katika picha ya pamoja muda mfupi baada ya kupokea tuzo ambayo kiwanda kimetunukiwa.

Baada ya kutumikiwa tuzo kubwa ya Mackay Award ya SABMiller kutokana na kufanya uzalishaji usiochafua mazingira hivi karibuni,wiki iliyopita kiwanda cha TBL cha Mwanza kuchomoza katika mashindano ya viwanda vya bia na kutangazwa kuwa ni kiwanda bora kinachoshikilia nafasi ya pili kwa ubora barani Afrika baada ya kushindanishwa na viwanda vingine 21 kutoka nchi mbalimbali.
Kiwanda cha TBL Mwanza ni kiwanda pekee barani Afrika ambacho kinatumia teknolojia ya uzalishaji wa kutumia pumba za mpunga hali ambayo imepunguza kasi ya uharibifu wa mazingira utokanao na mchakato wa uzalishaji viwandani.

Mbali na kutumia teknolojia hii rafiki kwa mazingira kiwanda hiki pia kimekuwa kinara kwa kuzalisha bidhaa bora na kimeleta chachu ya kukua kwa shughuli za kiuchumi katika Mkoa wa Mwanza ikiwemo kuongeza fursa za ajira za moja kwa moja na zisizo za moja kwa moja kwa wananchi bila kusahau kuendesha kampeni za matumizi mazuri ya maji na utunzaji wa mazingira.
Akiongelea mafanikio ambayo kiwanda kimeyapata,Richmond Raymond, aliyekuwa Meneja wa kiwanda hicho ambaye kwa sasa amehamishiwa  kikazi nchini Afrika ya Kusini alisema kuwa ushindi huu umetokana na Uwekezaji makini uliofanywa na kampuni bila kusahau juhudi za pamoja za wafanyakazi wake.

“Kushika nafasi kubwa kama hii barani Afrika sio jambo la mzaha,hii inadhihirisha kuwa watanzania tukiamua tunaweza na inawezekana dhamira ya serikali ya kuigeuza Tanzania nchi kuwa ya viwanda inaweza kutekelezeka.Tumekuwa tukitembelewa na wageni wengi kwenye viwanda vyetu kutoka sehemu mbalimbali kwa ajili ya kujua nini siri ya mafanikio yetu.Naamini tukishirikiana tunaweza kufanikiwa zaidi,mwisho nawashukuru wateja wetu wote wa mikoa ya kanda ya ziwa kwa kutuunga mkono na tutaendelea kuwaletea bidhaa bora na kushirikiana nao katika miradi mbalimbali ya kuleta mabadiliko kwa jamii na kuondoa umaskini.

No comments:

Post a Comment