METDO Tanzania

METDO Tanzania

Friday, September 23, 2016

HOSPITALI YA TAIFA MUHIMBILI KUPELEKA WATAALAMU SABA NCHINI INDIA KUJIFUNZA KWA VITENDO KUFANYA UPASUAJI


Na John Luhende, Dar es salaam

Hospital ya Taifa ya  Muhimbili imesema katika kutimiza azma ya serikali ya kupunguza idadi ya wagonjwa wanaokwenda nje  yanchi kutibiwa   ,septemba 25 mwakahuu itapeleka wataalam saba nchini India katika hospital ya Apollo Newdel ili kujifunza kwa vitendo kufanya upasuaji  nakupandikiza kifaa cha usikivu kwa watu wazima na watoto.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es salaam kaimu mkurugenzi wa hospital hiyo  Prof Lawrence Museru amesema  wataalamu hao watakaokwenda  ni pamoja na  madaktari  bingwa wawili wa upasuaji  wa pua, koo namaikio  ,wauguzi wawili wa chumba cha upasuaji,mtaalamu mmoja wa kupima usikivu pamoja na wataalamu wawili wakufundisha jinsi ya kuongea  kwa watoto Salio zaliwa na matatizo hayo.

Aidha  prof Museru amesema wataalamu hao wanatarajiwa kurejea okctoba 28 mwaka huu tayari kwa kuendelea kutoka Huduma hiyo na safari yao itagharimu  shilingi milioni 528 zikijumuishwa na gharama za  mafunzo,nauli ,gharama za kujikimu na za mafunzo mengine  na Hospital hiyo itagharamia hudua hizo.

 Amesema  kuwa Hospital hiyo inatarajia kutumia  kiasi cha shilingi billion 3.4 kwaajili ya kuongeza vyumba vya upasuaji kutoka 12 hadi   20 ambapo Sasa  wanafanya ukarabati wa Vyumba 12 vilivyopo  na kuweka vifaa vipya katika Vyumba vya upasuaji vitakavyo ongeza  eneo la Huduma za uchujaji wa damu kwa wagonjwa wa figo na kuongeza Vitanda  kutoka 17 vya Sasa hadi 42 pamoja na kuongeza  machine  kufikia 42 na kuwaeka mtambo wa kuchuja maji.

Museru ameeleza kuwa Hospitali pia itaongeza vyumba vipya vinne vya wagonjwa wenye kuhitaji uangalizi maalum (ICUs) vikiwa na Vitanda  40,vifaa maalumu na  vyumba 4 vya kupokea wagonjwa baada ya kutoka ICU (step- down ICU) vitanda 40 na ukarabati  wa miundombinu uta kamilika mwishoni mwa  mwaka huu.

Akijibuswali alilo ulizwa na waandishi kuhusu kutumia fedhanyingi kupeleka wataalamu nje kusoma badala ya kuleta waalimu wakawafundisha hapa hapa nchini prof Museru alisema

''Tanzania haiwezi kuwa Kisiwa  hasa kwa utaalam kama huu unaotuona hapa wote  tulijifunza kwa wenzetu na kupata uzoefu , wana  waeza kufunzwa hapa lakini waka  kosa uzoefu,  unapokuwa  huko unajifunza mengi hata nje ya masomo ila hata utendaji Kazi kwa vitendo" aliongeza  prof  Museru
Share:

0 comments:

Post a Comment

Copyright © WAZO HURU | Powered by Blogger Design by ronangelo | Blogger Theme by NewBloggerThemes.com