Na John Luhende, Dar es salaam
Hospital ya Taifa ya Muhimbili imesema katika kutimiza azma ya serikali ya kupunguza idadi ya wagonjwa wanaokwenda nje yanchi kutibiwa ,septemba 25 mwakahuu itapeleka wataalam saba nchini India katika hospital ya Apollo Newdel ili kujifunza kwa vitendo kufanya upasuaji nakupandikiza kifaa cha usikivu kwa watu wazima na watoto.
Aidha prof Museru amesema wataalamu hao wanatarajiwa
kurejea okctoba 28 mwaka huu tayari kwa kuendelea kutoka Huduma hiyo na
safari yao itagharimu shilingi milioni 528 zikijumuishwa na gharama za
mafunzo,nauli ,gharama za kujikimu na za mafunzo mengine na Hospital
hiyo itagharamia hudua hizo.
Amesema kuwa Hospital hiyo inatarajia kutumia kiasi cha
shilingi billion 3.4 kwaajili ya kuongeza vyumba vya upasuaji kutoka 12
hadi 20 ambapo Sasa wanafanya ukarabati wa Vyumba 12 vilivyopo na
kuweka vifaa vipya katika Vyumba vya upasuaji vitakavyo ongeza eneo la
Huduma za uchujaji wa damu kwa wagonjwa wa figo na kuongeza Vitanda
kutoka 17 vya Sasa hadi 42 pamoja na kuongeza machine kufikia 42 na
kuwaeka mtambo wa kuchuja maji.
Museru ameeleza kuwa Hospitali pia itaongeza vyumba vipya
vinne vya wagonjwa wenye kuhitaji uangalizi maalum (ICUs) vikiwa na
Vitanda 40,vifaa maalumu na vyumba 4 vya kupokea wagonjwa baada ya
kutoka ICU (step- down ICU) vitanda 40 na ukarabati wa miundombinu uta
kamilika mwishoni mwa mwaka huu.
Akijibuswali alilo ulizwa na waandishi kuhusu kutumia
fedhanyingi kupeleka wataalamu nje kusoma badala ya kuleta waalimu
wakawafundisha hapa hapa nchini prof Museru alisema
''Tanzania haiwezi kuwa Kisiwa hasa kwa utaalam kama huu
unaotuona hapa wote tulijifunza kwa wenzetu na kupata uzoefu , wana
waeza kufunzwa hapa lakini waka kosa uzoefu, unapokuwa huko
unajifunza mengi hata nje ya masomo ila hata utendaji Kazi kwa vitendo"
aliongeza prof Museru
No comments:
Post a Comment