Utafiti unaonyesha zao la mipapai ni zao ambalo halihitaji na halina
gharama kubwa lakini faida yake ni kubwa sana. heka moja inachukuwa
miche ya mipapai kati ya 400 au 600. mbegu zinapatikana katika kila duka
la pembejeo.Pia unaweza
kununua papai sokoni ukalila alafu mbegu ukazihifadhi kwa ajili ya
kuzipanda baadae. mara nyingi mpapai hauhitaji mbolea lakini inategemea
na ardhi yenyewe. mpapai unatumia miezi kati ya 9 mpaka 15 kuanza
kuvuna.
Kadri mpapai unavyokaa muda mrefu ndivyo unavyodhidi kuzaa zaidi. mpapai
kwa kadilio la.chini unatoa mapapai si chini ya 9 kwa kadirio la chini.
pia mapapai yanaiva kwa kipindi. hivyo mapapai yanavyokomaa mara nyingi
yanaiva matatu matatu mpaka manne kwa mpapai mmoja.
Sasa basi kama mpapai mmoja utakuwa unavuna mapapai manne ukizidisha
mara miche uliyopanda kwa heka moja mfano miche 500. kwahiyo 4x500
utapata mapapai 2000 ukiuza kwa kila moja tshs. 500 tu. utapata tshs.
1,000,000 na hapo umevuna round moja tu. na kwa msimu unavuna mpaka
round 4 kwa 7 . utakuwa na tshs. ngapi? pia zao hili halisumbui kabisa.
pia mpapai unavunwa mpaka miaka 3 hadi 5 kabla haujazeeka.
Pia kwenye shamba la mipapai unaweza kupanda na mbogamboga. sasa hizo
hesabu ni kwa heka 1 tu. je aliyepanda heka 2 mpaka 5 na kuendelea?
mahitaji ya mapapai sokoni ni makubwa kuliko yanayozarishwa sasa. KATAA
UMASIKINI SASA. wekeza kwa ajili yako na uzao wako.
MAHITAJI
Hali ya hewa inayofaa kwa mipapai ni ya kitropik ambayo haina baridi
kali na joto kiasi . Udongo usiotuamisha maji maji yakisimama kwa masaa
48 tu mpapai unaweza kufa, wenye ruruba ya kutosha kwa sababu mipapai
haina mzizi mkuu haihiyaji udongo wenye kina kirefu, kipindi cha jua
kali mpapai usiachwe zaidi ya wiki 8 bila kumwagiliwa maji kama hakuna
mvua ingawa wakati wa mapapai kuiva kama kuna ukame basi hii huongeza
ubora wa papai ikiwamo kutooza mapema sokoni
Mipapai ipandwe sehemu ambazo hazina upepo mwingi kwani huvunjika
kirahisi, kama unashamba la mipapai itakubidi kupanda miti ya kukinga
upepo kuzunguka shamba lako, miti kama miparachichi, migravilea,
vibiriti (leucaena Spp) na miembe pia inafaa. Hakikisha miti ya kukinga
upepo inakuwa mirefu kuzidi mipapai kwa mita 10 mpaka 20 juu zaidi
Kuendelea kupanda mipapai kwenye shamba moja kunaweza kusababisha usugu
wa magonjwa, nashauri baada ya miaka 3 – 5 ubadilishe zao hili angalau
kwa msimu mmoja ili kuua mzunguko wa magonjwa.
Mipapai inaweza kuchanganganywa na miembe na mimea jamii ya michungwa,
pia mazao ya msimu kama mahindi, mtama, ufuta , alizeti na mboga mboga
yanaweza kulimwa. Kwa kaida kwenye mipapai kuna mipapai dume, majike
na yenye jinsia zote (multiplesex/hermaphrodite) ambayo huwa na mapapai
marefu zaidi, na pia kuna isiyoeleweka ambayo huwa na mapapai mafupi
sana
MBEGU
Kusanya mbegu toka kwenye mapai makubwa na yaliyo komaa na kuiva, kausha
mbegu vizuri kbla ya kupanda, kama utapata mbegu za kununua ni vizuri
zaidi, baada ya kukausha hakikisha unazipanda ndani ya wiki moja Ila
unashauriwa kutumiwa mbegu za hybreed chotara
KUOTESHA MBEGU
Kuna wanaopendelea kuotesha mbegu kwanza na kisha kuhamishia miche
shambani, sehemu ya kuoteshea iandaliwe miezi miwili kabla, mbegu
zioteshwe kwenye kina kati ya sentimeta 1 – 2 chini ya udongo wenye
rutuba au pakiti za plastiki, kiwango bora cha joto ni sentigredi 21 –
27 na itachukua kati ya wiki 1 – 4 kwa mbegu kuota, kwenye kila pakiti
weka mbegu 2 – 3. Panda mbegu zako kwenye kitalu kwa umbali wa sentimeta
3 toka shimo hadi shimo na sentimeta 15 kati ya mistari, hakikisha maji
hayatuami kabisa, pia unaweza kupiga dawa ya copper oxychloride gramu
moja katika lita moja ya maji ilikukinga miche yako na fangasi
UOTESHAJI WA MOJA KWA MOJA
Kabla ya kupanda mbegu weka mchanganyiko wa majivu na mbolea ya kuku
sehemu ya kupandia, mbolea husaidia ukuaji haraka na jivu husaidia
kukinga mipapai na magonjwa. Panda mbegu 3 – 5 kila shimo maana miche
mingine inaweza kufa kwa magonjwa, kuliwa na wadudu au ikaota dume
KUHAMISHA MICHE TOKA KWENYE KITALU
Miche ihamishiwe shambani ikiwa na urefu wa sentimeta 20 – 40, kama
udongo unatuamisha maji panda kwenye matuta yenye urefu wa sentimeta 40 –
60 mashimo yawe na ukubwa wa sentimeta 45 upana na sentimeta 30 kina na
shimo lichanganywe na udongo na samadi bila kuacha kisahani cha maji,
umbali ni mita 3 kwa 3 kwani mipapai inahitaji jua la kutosha.
KUPUNGUZA MIPAPAI
Baada ya miezi 3 – 5 baada ya kupanda mipapai itatoa maua na hapo jinsia
ya mipapai itajulikana na mingine itabidi ipunguzwe na hasa midume,
mipapai yenye jinsi zote inatakiwa isizidi asilimia 10 – 20 na midume
ibaki mmoja katika kila mijike 25, mimea yenye magonjwa pia inabidi
ing’olewe.
RUTUBA YA UDONGO
Weka kiasi chakilo 2 – 5 za samadi kwenye kila mpapai kwa mwaka ili
kuongeza ukuaji na uzazi, mabaki ya mimea yanaweza pia kuwekwa kama
matandazo na h ii ni muhimu zaidi kipindi cha kiangazi ili kuzuia unyevu
usipotee.
MAGUGU
Mipapai inapopandwa tu inaweza kuwekewa matandazo kuizunguka ili kuzuia
uoataji wa magugu, magugu yang’olewe yakiwa machanga na epuka kuchimbua
chini sana maana mizizi ya mipapai huwa juu juu, njia nzuri ni kuweka
matandazo kwenye shamba lote ili kuzuia outaji wa magugu
UANGALIZI
Mipapai iangaliwe dhidi ya magonjwa, ing’olewe na kuchomwa au kufukiwa
chini ikiwa itabainika kuwa na maonjwa, piga dawa dhidi ya magonjwa ya
fangasi na virusi mara yanapoibuka ili kuongeza uzaaji nakipato chako.
Ondoa matawi yote yatakayojitokeza pembeni ya mpapai wako, na hii
ifanyike mapema kabla ya tawi kuwa kubwa.
Ondoa mapapi yote ambayo yatakuwa hayakuchavuliwa vizuri na acha yale
yenye afya tu Weka miti ya kuegemea kama mpapai utazaa matunda mengi na
hasa wakati wa upepo mwingi ili kuzuia mipapai isivunjike. Mipapai
ikitunzwa inaweza kuishi mika mingi, ila kwa ajili ya mazao bora ondoa
mipapai na upande mingine baada ya kila miaka mitatu (3)
FAIDA
Papai zao zuri sana na kama ukipanda eka moja kwa 1000 mapapai utapata
1kila wiki, ukiuza 1000 kwa 300 tu ni laki 3 sasa ukiweka eka 5 ni 1.5m
kwa wiki...dahhhh....Tanzania nzuri unataka kendwa wapi.
Thursday, September 29, 2016
KARIBU TUME YA MAENDELEO YA USHIRIKA
Popular Posts
-
📌 Asema Rais, Dkt. Samia anafanya kazi kubwa ya kuwaunganisha Watanzaia 📌 Atak...
-
Katibu Mkuu wa Wizara ya kilimo Mhandisi Mathew Mtigumwe Na Mathias Canal, Wizara ya Kilimo-Dodoma Katibu Mkuu wa Wizara ya kilim...
-
Kaimu mkurugenzi mkuu wa kituo cha uwekezaji Tanzania (TIC) Clifford Tandari Julia akizungumza na waandishi wa habari hawapo pichani alik...
-
Na Mathias Canal, WEST-Rombo Ndizi ni zao kubwa la biashara na chakula hivyo likitumika vizuri litabadili uchumi wa wakulima na nchi kwa uju...
Powered by Blogger.
0 comments:
Post a Comment