Na.John Luhende
Kituo cha uwekezaji kimesema hatua ya serikali kuhamishia makao makuu yake mkoani Dodoma kumefungua fursa nyingi za uwekezaji katika mikoa jirani hasa mkoani Morogoro ambao una eneo kubwa linalo faa kwa uwekezaji wa kilimo, na viwanda.
Akizungumza na waandishi wa habari kaimu mkurugenzi wa
kituo hicho Clifford Tandari amesema kituo cha uwekezaji nchini kwa
kushirikiana na mkoa wa Morogoro wame andaa mkutano Mkubwa wa
kuhamasisha na kukuza uwekezaji na biashara mkoani huko mwishoni mwa
mwezi huu.
Amesema,Kituo hicho mpaka Sasa kimweweza kusaji miradi 198
ambapo vote itaelekezwa mkoani Morogoro na inatarajiwa kuzalisha ajira
ziapatazo 28,944 ambapo ambapo katika miradi 111 ni ya watanzania
,miradi 41 ni ya wageni na miradi 46 ni ya ubia kati ya wageni na
watanzania.
Naye mkuu wa mkoa wa Morogoro Kebwe Steven Kebwe amesema
mkoa huo umejaaliwa kuwa na fursa na mazingira mazuri ya uwekezaji,na
lasili Mali nyingi ambazo bado hazija tumika ipasavyo na wakati umefika
Sasa kwa wawekezaji kuchangamkia fursa hiyo.
0 comments:
Post a Comment