NA Beatrice Lyimo-MAELEZO
WAZIRI wa
Mambo ya ndani ya nchi Mwigulu Nchemba anatarajia kuwa mgeni rasmi
katika Mkutano Mkuu wa Mwaka wa 47 wa Jumuiya ya Waislamu wa Ahmadiyya
utakaofanyika kuanzia Septemba 30 hadi Octoba 2 mwaka huu.
Akizungumza
kwa niaba ya Mkuu wa Jumuiya hiyo Sheikh Tahir Mahmood Chaudhry, Katibu
Mkuu Msaidizi Abdurahman Ame alisema kuwa mkutano huo utafanyika eneo
la kitonga, kata ya Msongola Manispaa ya Ilala jijini Dar es Salaam.
Alisema
Jumuiya imeandaa mkutano huo kwa lengo la kuhamasisha amani katika jamii
na kuwakumbusha waumini hasa wa kiislamu juu ya misingi sahihi ya dini
ya kiislamu pamoja na kumjua na kutimiza haki ya Mwenyezi Mungu.
“Wajibu
wa kiongozi wa dini ni kuandaa na kuhamasisha masuala ya dini, hivyo
lengo la mkutano huo ni kuhamasisha amani katika jamii na pia
kuwakumbusha waumini wa kiislamu juu ya kumjua, kuishi na kutimiza haki
ya Mwenyezi Mungu hali itakayosaidia kuondokana na vitendo viovu,”
alifafanua Katibu huyo.
Mbali na
hayo, mkutano huo utabebwa na kaulimbiu isemayo “kuitambua amani ya
jirani yako, huvunjilia mbali kuta zinazowatenganisha” ikiwa na ujumbe
ya kwamba kuna haja ya kuelimisha jamii uzuri wa mafundisho ya dini kwa
kutumia vitabu vitakatifu kupitia vyombo mbalimbali vya masasiliano.
Vile
vile, Washiriki mbalimbali kutoka ndani na nje ya nchi zikiwemo Kenya,
Uganda, Burundi, Malawi, Msumbiji na Uingereza wakiwemo viongozi wa
vyama vya siasa, taasisi za kidini na za kijamii watashiriki katika
mkutano huo.
0 comments:
Post a Comment