“Mratibu
wa Taifa wa Muungano wa Utepe Mweupe wa Uzazi Salama, Bi. Rose Mlay
(katikati) akizungumza na waandishi wa habari waliohudhuria semina juu
ya namna ya mamlaka husika kukabiliana na matukio ya vifo vinavyotokana
na uzazi.”
Meneja
Mradi wa Muungano wa Utepe Mweupe wa Uzazi Salama (WRATZ), Sizarina
Hamisi (kushoto) akiwasilisha mada katika semina hiyo kwa wanahabari.
Ofisa Habari wa Muungano wa Utepe Mweupe wa Uzazi Salama (WRATZ), Robert Zephania akizungumza katika semina hiyo.
Chiku
Lweno (kulia) akiwasilisha mada kwa waandishi wa habari waliohudhuria
semina iliyoandaliwa na Muungano wa Utepe Mweupe wa Uzazi Salama
(WRATZ).
IMEELEZWA
kwamba utashi wa Rais wa Tanzania, Dk. John Pombe Magufuli na moyo wa
huruma atakaouonesha juu ya matukio ya vifo vitokanavyo na uzazi ni
suluhisho la kudumu la janga la vifo hivyo ambavyo kila siku vimekuwa
vikipoteza maisha ya mama na mtoto.
Kauli
hiyo imetolewa leo jijini Dar es Salaam na Mratibu wa Taifa wa Muungano
wa Utepe Mweupe wa Uzazi Salama, Bi. Rose Mlay kwenye semina kwa
waandishi wa habari kutoka vyombo mbalimbali vya habari ikiwa ni
kuwajengea uwezo wanahabari hao kupaza sauti juu ya kukabiliana na vifo
vinavyotokana na uzazi kwa wajawazito.
Bi. Mlay
alisema endapo Rais Magufuli atatamka kuanzia jana kuwa hataki kusikia
matukio ya vifo vitokanavyo na uzazi vinaweza kudhibitiwa na
vikatokomea. Alisema vifo hivyo vinaweza kuzuilika endapo akinamama wote
wanaopata matatizo ya uzazi watapatiwa huduma kamili za uzazi za
dharura kwa wakati na wataalamu stahiki.
“…Nasema
hivyo kwa sababu Mh. Rais akitamka jana hii kwamba kuanzia leo hataki
kusikia kifo hata kimoja cha mwanamke kinatokea kutokana na matatizo ya
uzazi, basi itakuwa hivyo. Hii ni kwa sababu vifo hivi vinazuilika kama
kinamama wote wanaopata matatizo ya uzazi watapatiwa huduma kamili za
uzazi za dharura ni jambo muhimu hapa kwa sababu matatizo
yanayosababisha vifo hayasubiri,” alisema Bi. Mlay.
Alisema
takwimu zinaonesha kwa kila uchao takribani akinamama 24 wanakufa kwa
matatizo ya uzazi nchini kwa kile kukosa huduma kamili za uzazi za
dharura stahiki, jambo ambalo linaweza kudhibitiwa endapo maamuzi
yatafanywa na mamlaka husika.
0 comments:
Post a Comment