Friday, August 19, 2016

Utashi wa Rais Magufuli suluhisho la vifo vinavyotokana na uzazi nchini

JPG
“Mratibu wa Taifa wa Muungano wa Utepe Mweupe wa Uzazi Salama, Bi. Rose Mlay (katikati) akizungumza na waandishi wa habari waliohudhuria semina juu ya namna ya mamlaka husika kukabiliana na matukio ya vifo vinavyotokana na uzazi.”
Meneja Mradi wa Muungano wa Utepe Mweupe wa Uzazi Salama (WRATZ), Sizarina Hamisi (kushoto) akiwasilisha mada katika semina hiyo kwa wanahabari.
Meneja Mradi wa Muungano wa Utepe Mweupe wa Uzazi Salama (WRATZ), Sizarina Hamisi (kushoto) akiwasilisha mada katika semina hiyo kwa wanahabari.
Ofisa Habari wa Muungano wa Utepe Mweupe wa Uzazi Salama (WRATZ), Robert Zephania akizungumza katika semina hiyo.
Ofisa Habari wa Muungano wa Utepe Mweupe wa Uzazi Salama (WRATZ), Robert Zephania akizungumza katika semina hiyo.
Chiku Lweno (kulia) akiwasilisha mada kwa waandishi wa habari waliohudhuria semina iliyoandaliwa na Muungano wa Utepe Mweupe wa Uzazi Salama (WRATZ).
Chiku Lweno (kulia) akiwasilisha mada kwa waandishi wa habari waliohudhuria semina iliyoandaliwa na Muungano wa Utepe Mweupe wa Uzazi Salama (WRATZ).

IMEELEZWA kwamba utashi wa Rais wa Tanzania, Dk. John Pombe Magufuli na moyo wa huruma atakaouonesha juu ya matukio ya vifo vitokanavyo na uzazi ni suluhisho la kudumu la janga la vifo hivyo ambavyo kila siku vimekuwa vikipoteza maisha ya mama na mtoto.

Kauli hiyo imetolewa leo jijini Dar es Salaam na Mratibu wa Taifa wa Muungano wa Utepe Mweupe wa Uzazi Salama, Bi. Rose Mlay kwenye semina kwa waandishi wa habari kutoka vyombo mbalimbali vya habari ikiwa ni kuwajengea uwezo wanahabari hao kupaza sauti juu ya kukabiliana na vifo vinavyotokana na uzazi kwa wajawazito.

Bi. Mlay alisema endapo Rais Magufuli atatamka kuanzia jana kuwa hataki kusikia matukio ya vifo vitokanavyo na uzazi vinaweza kudhibitiwa na vikatokomea. Alisema vifo hivyo vinaweza kuzuilika endapo akinamama wote wanaopata matatizo ya uzazi watapatiwa huduma kamili za uzazi za dharura kwa wakati na wataalamu stahiki.

“…Nasema hivyo kwa sababu Mh. Rais akitamka jana hii kwamba kuanzia leo hataki kusikia kifo hata kimoja cha mwanamke kinatokea kutokana na matatizo ya uzazi, basi itakuwa hivyo. Hii ni kwa sababu vifo hivi vinazuilika kama kinamama wote wanaopata matatizo ya uzazi watapatiwa huduma kamili za uzazi za dharura ni jambo muhimu hapa kwa sababu matatizo yanayosababisha vifo hayasubiri,” alisema Bi. Mlay.

Alisema takwimu zinaonesha kwa kila uchao takribani akinamama 24 wanakufa kwa matatizo ya uzazi nchini kwa kile kukosa huduma kamili za uzazi za dharura stahiki, jambo ambalo linaweza kudhibitiwa endapo maamuzi yatafanywa na mamlaka husika.

Aidha Mratibu huyo wa Taifa wa Muungano wa Utepe Mweupe wa Uzazi Salama alieleza hali hiyo inaweza kudhibitiwa endapo wilaya zote zinatoa kipaumbele na kutenga fungu pekee la huduma kamili za uzazi za dharura na kuzilinda kuhakikisha zinatumika kwa makusudio yaliyowekwa. Bajeti za halmashauri zitumwe kwa wakati mara zinapopitishwa ili ziweze kutumika kwa wakati na kutatua changamoto hizo.

No comments:

Post a Comment