METDO Tanzania

METDO Tanzania

Thursday, August 18, 2016

MGODI WA DHAHABU WA BULYANHULU WATENGENEZA AJIRA KWA WAJASILIAMALI VIJIJINI

K31A8729
Afisa Mahusiano wa Mgodi wa Bulayanhulu Sara Teri (kulia) na Meneja wa Ufanisi wa Mgodi wa Bulayanhulu Elias Kasitila wakikabidhi madawati kwa Mkuu wa Wilaya ya Nyang’wale Hamim Gwiyama pamoja na viongozi wengine wa Wilaya ya Nyangw’ale.

Meneja wa Ufanisi wa Mgodi wa Bulyanhulu uliopo mkoani Geita ,Elias Kasitila akizungumza katika hafla ya makabidhiano ya madawati yaliyotolewa na mgodi huo kwa ajili ya shule zilizoko katika wilaya ya Nyang’wale.

Utengenezaji wa Madawati ulitoa fursa ya ajira kwa fundi Deus Mlela aliyepewa tenda na Mgodi wa Bulyahulu ya kutengeneza madawati mia tano.


Fursa ya ajira iliendelea kusambaa kwa dereva wa trekta Bw ,Machibya aliyepata tenda ya kusafirisha Madawati kwenda katika shule zilizokusudiwa kupata Madawati hayo.

Lakini pia wakati wa shughuli za utengezaji wa Madawati hayo mafundi walihitaji kupata chakula na hii pia ikawa Fursa kwa Mama Nitilie Devotha Sonda wa Sonda ambaye alikuwa akitoa huduma ya chakula kwa mafundi hao.

Mgodi wa dhahabu wa Bulyanhulu umetengeneza mamia ya ajira kwa vijana na wanawake wanaoishi maeneo mbalimbali mkoani shinyanga na Geita kupitia mpango wa kutengeneza madawati elfu sita katika maeneo mbalimbali ya mikoa hiyo yenye thamani ya shilingi milioni 200.

Wakizungumza kwa nyakati tofauti vijana wamesema neema ya kujiingizia vipato kwa kushiriki kwenye shughuli mbalimbali katika zoezi la kutengeneza madawati imebadili maisha yao hasa katika msimu huu wa kiangazi ambao wengi wao ajira zao zimesimama kwani walio wengi wanategemea mvua kwenye ajira yao ya msingi ya kilimo.

“Tunashukuru sana msimu huu wa kiangazi, tumepata nafasi ya kupata kazi za ambazo zinatupatia kipato kupitia utengenezaji wa madawati, mimi hapa ni fundi chuma, nachomelea vyuma na kazi yangu hii huku vijijini wateja ni wachache sana, muda mwingi huwa tuko doro kwenye kijiwe chetu lakini sasa hivi tuna kazi nyingi sana za kutengeneza madawati hapa imebidi niajiri vijana wengine watano kuweza kunisaidia kukamilisha kazi ya kuunganisha vyuma kwa ajili ya madawati mia tano ambayo tumepata tenda na Kampuni iliyoshinda tenda ya kutengeneza madawati kwa gharama ya mgodi wa dhahabu ya Bulyanhulu.” Anasema Abbas Mbua mkazi wa kata ya Msalala wilaya ya Nyang’wale mkoani Geita.

“Sisi wapiga msasa tunajipatia shilingi elfu kumi na tano kwa kila dawati 5 hii si haba, kiasi hiki kimenisaidia sana maana sikupata vizuri mazao mwaka huu kwa hiyo pesa niliyoingiza kwenye kazi ya kupiga msasa imebadili kabisa hali halisi nyumbani, nimenunua gunia za mahindi, maharage na mchele, hali imetulia kwa kweli siwezi kusema uongo” anasema Maige Deus mkazi wa Kahama.

“Ninaiomba sana serikali yetu iendelee kuvumbua miradi mingine ili sisi vijana tuendelee kuchapa kazi, maana vinginevyo tunakaa vijiweni kazi hamna, lakini mradi huu wa madawati ulivyokuja hatuna hata muda wa kuvuta sigara, tuko bize kutwa nzima tunatengeneza madawati, hapa mimi ndiyo fundi mkuu kwenye hiki kiwanda naunganisha mbao na kuhakikisha madawati yako vizuri kwa ajili ya wanafunzi.” Anasema Abdul Karim Ramadhani akiwa katika kiwanda cha Zacharia and Deus Timber Supply cha Nyang’wale mkoani Geita.

Halikadharika mama nilitie nao wanasema si haba mradi wa kuchonga madawati umeongeza idadi ya wateja katika migahawa yao, Devotha Sonda wa Sonda Mama Nitiliea katika kijiji cha Msalala anasema “ Kabla ya mradi wa madawati vyakula hapa tulikwa tunapika kidogo na wateja walikuwa ni wa kubangaiza tu lakini sasa hivi kutokana  uchongaji wa madawati vijana ni wengi sana na binafsi nimepewa tenda kabisa ya kupikia vijana wanaotengeneza madwati na ninalipwa vizuri na kwa muda, naomba miradi kama hii iendelee tu hadi madawati yatoshe na sisi mitaji itakuwa imekua. Mwaka huu maswala ya ada kwa watoto, mavazi sasa ni jambo rahisi.”

Naye Mkurugenzi wa kampuni ya kizawa ya Zacharia and Deus Timber Supply Deus Mlela iliyopo Nyang’wale kilomita hamsini kutoka mgodi wa Bulyanhulu amesema, “Tenda ya kutengeneza madawati mia tano kutoka Bulyanhulu kwetu tumepata faida mara mbili kwanza imetuongezea mtaji na pili imetupa uwezo na kujulikana kwa wadau wengine, sasa hivi tumepatiwa tena tenda na Halamashauri ya wilaya kutengeneza madawati mengine elfu moja na kampuni nyingine imetupa tenda na madawati mia mbili, bila kazi ya Bulyanhulu kutufungulia mlango ingekuwa vigumu kuweza kupokea tenda hizo kwa sababu mtaji ulikuwa mdogo. Tunaomba wadau waendelee kutuamini ili na sie tuweze kuendelea kusambaza ajira kwa vijana ambao hawana ajira.

Naye Mkuu wa Wilaya ya Nyang’wale Hamim Gwiyama amesema, “Kimsingi kuwa karibu na Mgodi wa dhahabu wa Bulyanhulu imewafanya watu wa Nyang’wale ule uzito wa kazi ya madawati kuwa tofauti na sehemu nyingine, japo hatujamaliza kabisa tuna mapungufu kidogo, faida ya mradi wa madati faida yake ya kwanza ni kwa watoto wa shule ambayo ni walengwa, wanapata madawati wake vizuri na waweze kuelewa masomo yao vizuri,  kwa njia nyingine mpango huu umetengeneza ajira, wale watengeneza mawadaati wamepata kazi ya kufanya na kipato, wanajipatia mahitaji wengine wananunua mifugo, kwa mfano katika mradi huu bulyanhulu imedhamini madawati yenye thamani ya shilingi million thethini na tano na hii pesa imezunguka kwa watu wote, mafundi seremala, waendesha mikokoteni, mama nitilie, na wengine wengi wamejipatia kipato na hata mitaji.”

Mwaka 2013 Mgodi wa Bulyanhulu ulitoa madawati 1329 kwa ajili ya shule 10 za msingi  zinazozunguka mgodi  wa Bulyahulu.

Mwaka huu 2016 Madawati 1380 kwa halmashauri ya Msalala madawati  500 kwa wilaya ya Nyang’wale 500, madawati 2000 yatatolewa hivi karibuni kwa mkoa wa Shinyanga na pia Bulyanhulu itaipatia dola za kimarekani elfu 6000 shule ya msingi ya binafsi ya St. JosephineBhakita iliyoko km 12 kutoka mgodi wa dhahabu wa Bulyanhulu katika kijiji cha Ilogi kata ya Bulyanhulu.
Share:

0 comments:

Post a Comment

Copyright © WAZO HURU | Powered by Blogger Design by ronangelo | Blogger Theme by NewBloggerThemes.com