Afisa Mahusiano wa Mgodi wa Bulayanhulu Sara Teri (kulia) na Meneja wa Ufanisi wa Mgodi wa Bulayanhulu Elias Kasitila wakikabidhi madawati kwa Mkuu wa Wilaya ya Nyang’wale Hamim Gwiyama pamoja na viongozi wengine wa Wilaya ya Nyangw’ale.
Meneja wa
Ufanisi wa Mgodi wa Bulyanhulu uliopo mkoani Geita ,Elias Kasitila
akizungumza katika hafla ya makabidhiano ya madawati yaliyotolewa na
mgodi huo kwa ajili ya shule zilizoko katika wilaya ya Nyang’wale.
Utengenezaji
wa Madawati ulitoa fursa ya ajira kwa fundi Deus Mlela aliyepewa tenda
na Mgodi wa Bulyahulu ya kutengeneza madawati mia tano.
Fursa ya
ajira iliendelea kusambaa kwa dereva wa trekta Bw ,Machibya aliyepata
tenda ya kusafirisha Madawati kwenda katika shule zilizokusudiwa kupata
Madawati hayo.
Lakini
pia wakati wa shughuli za utengezaji wa Madawati hayo mafundi walihitaji
kupata chakula na hii pia ikawa Fursa kwa Mama Nitilie Devotha Sonda wa
Sonda ambaye alikuwa akitoa huduma ya chakula kwa mafundi hao.
Mgodi wa dhahabu wa Bulyanhulu umetengeneza mamia ya ajira kwa vijana na wanawake wanaoishi maeneo
mbalimbali mkoani shinyanga na Geita kupitia mpango wa kutengeneza
madawati elfu sita katika maeneo mbalimbali ya mikoa hiyo yenye thamani
ya shilingi milioni 200.
Wakizungumza kwa nyakati tofauti vijana wamesema neema ya kujiingizia vipato kwa kushiriki kwenye shughuli mbalimbali katika zoezi la kutengeneza madawati imebadili maisha yao hasa katika msimu huu wa kiangazi ambao wengi wao ajira zao zimesimama kwani walio wengi wanategemea mvua kwenye ajira yao ya msingi ya kilimo.
“Tunashukuru sana msimu huu wa kiangazi, tumepata nafasi ya kupata kazi za ambazo zinatupatia kipato
kupitia utengenezaji wa madawati, mimi hapa ni fundi chuma, nachomelea
vyuma na kazi yangu hii huku vijijini wateja ni wachache sana, muda
mwingi huwa tuko doro kwenye kijiwe chetu lakini sasa hivi tuna kazi
nyingi sana za kutengeneza madawati hapa imebidi niajiri vijana wengine
watano kuweza kunisaidia
kukamilisha kazi ya kuunganisha vyuma kwa ajili ya madawati mia tano
ambayo tumepata tenda na Kampuni iliyoshinda tenda ya kutengeneza
madawati kwa gharama ya mgodi wa dhahabu ya Bulyanhulu.” Anasema Abbas
Mbua mkazi wa kata ya Msalala wilaya ya Nyang’wale mkoani Geita.
“Sisi
wapiga msasa tunajipatia shilingi elfu kumi na tano kwa kila dawati 5
hii si haba, kiasi hiki kimenisaidia sana maana sikupata vizuri mazao
mwaka huu kwa hiyo pesa niliyoingiza kwenye kazi ya kupiga msasa
imebadili kabisa hali halisi nyumbani, nimenunua gunia za mahindi,
maharage na mchele, hali imetulia kwa kweli siwezi kusema uongo” anasema
Maige Deus mkazi wa Kahama.
“Ninaiomba sana serikali yetu iendelee kuvumbua miradi mingine ili sisi vijana tuendelee kuchapa
kazi, maana vinginevyo tunakaa vijiweni kazi hamna, lakini mradi huu wa
madawati ulivyokuja hatuna hata muda wa kuvuta sigara, tuko bize kutwa
nzima tunatengeneza madawati, hapa mimi ndiyo fundi mkuu kwenye hiki
kiwanda naunganisha mbao na kuhakikisha madawati yako vizuri kwa ajili
ya wanafunzi.” Anasema Abdul Karim Ramadhani akiwa katika kiwanda cha
Zacharia and Deus Timber Supply cha Nyang’wale mkoani Geita.
Halikadharika mama nilitie nao wanasema si haba mradi wa kuchonga madawati umeongeza idadi ya wateja
katika migahawa yao, Devotha Sonda wa Sonda Mama Nitiliea katika kijiji
cha Msalala anasema “ Kabla ya mradi wa madawati vyakula hapa tulikwa
tunapika kidogo na wateja walikuwa ni wa kubangaiza tu lakini sasa hivi
kutokana uchongaji wa madawati vijana ni wengi sana na binafsi nimepewa
tenda kabisa ya kupikia vijana wanaotengeneza madwati na ninalipwa
vizuri na kwa muda, naomba miradi kama hii iendelee tu hadi madawati
yatoshe na sisi mitaji itakuwa imekua. Mwaka huu maswala ya ada kwa
watoto, mavazi sasa ni jambo rahisi.”
Naye Mkurugenzi wa kampuni ya kizawa ya Zacharia and Deus Timber Supply Deus Mlela iliyopo Nyang’wale
kilomita hamsini kutoka mgodi wa Bulyanhulu amesema, “Tenda ya
kutengeneza madawati mia tano kutoka Bulyanhulu kwetu tumepata faida
mara mbili kwanza imetuongezea mtaji na pili imetupa uwezo na kujulikana
kwa wadau wengine, sasa hivi tumepatiwa tena tenda na Halamashauri ya
wilaya kutengeneza madawati mengine elfu moja na kampuni nyingine
imetupa tenda na madawati mia mbili,
bila kazi ya Bulyanhulu kutufungulia mlango ingekuwa vigumu kuweza
kupokea tenda hizo kwa sababu mtaji ulikuwa mdogo. Tunaomba wadau
waendelee kutuamini ili na sie tuweze kuendelea kusambaza ajira kwa
vijana ambao hawana ajira.
Naye Mkuu wa Wilaya ya Nyang’wale Hamim Gwiyama amesema, “Kimsingi kuwa karibu na Mgodi wa dhahabu
wa Bulyanhulu imewafanya watu wa Nyang’wale ule uzito wa kazi ya
madawati kuwa tofauti na sehemu nyingine, japo hatujamaliza kabisa tuna
mapungufu kidogo, faida ya mradi wa madati faida yake ya kwanza ni kwa
watoto wa shule ambayo ni walengwa, wanapata madawati wake vizuri na
waweze kuelewa masomo yao vizuri, kwa njia nyingine mpango huu
umetengeneza ajira, wale watengeneza mawadaati wamepata kazi ya kufanya
na kipato, wanajipatia mahitaji wengine wananunua mifugo, kwa mfano
katika mradi huu bulyanhulu imedhamini madawati yenye thamani ya
shilingi million thethini na tano na hii pesa imezunguka kwa watu wote,
mafundi seremala, waendesha mikokoteni, mama nitilie, na wengine wengi
wamejipatia kipato na hata mitaji.”
Mwaka 2013 Mgodi wa Bulyanhulu ulitoa madawati 1329 kwa ajili ya shule 10 za msingi zinazozunguka mgodi wa Bulyahulu.
No comments:
Post a Comment