Rais wa
Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein
(katikati) pamoja na Viongozi wengine na wananchi wakibeba jeneza la
Marehemu Mzee Hamid Ameir Muasisi wa Mapinduzi,pia Mwenyekiti wa Baraza
la Wazee wa CCM baada ya kuswaliwa jana wakati wa Mazishi yake
yaliyofanyika Kijijini kwao Donge wilaya ya Kaskazini B.Unguja,[Picha na
Ikulu.]
Wananchi
waliohudhuria katika mazishi ya Marehemu Mzee Hamid Ameir Muasisi wa
Mapinduzi,pia Mwenyekiti wa Baraza la Wazee wa CCM
wakilibeba jeneza wakati wa Mazishi yake yaliyofanyika jana Kijijini
kwao Donge wilaya ya Kaskazini B.Unguja,[Picha na Ikulu.]
Rais wa
Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein
(katikati) akitia udongo katika kaburi la Marehemu Mzee Hamid Ameir
Muasisi wa Mapinduzi,pia Mwenyekiti wa Baraza la Wazee wa CCM baada ya
kufariki jana katika hospitali ya Mnazi Mmoja na kuzikwa jana Kijijini
kwao Donge wilaya ya Kaskazini B.Unguja,[Picha na Ikulu.]
Rais wa
Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein
(katikati) pamoja na wananchi na Viongozi wakiwa katika maziko ya
Marehemu Mzee Hamid Ameir Muasisi wa Mapinduzi,pia Mwenyekiti wa Baraza
la Wazee wa CCM aliyezikwa jana Kijijini kwao Donge wilaya ya Kaskazini
B.Unguja,[Picha na Ikulu.]
Rais wa
Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein
(katikati) pamoja na Viongozi wengine na wananchi wakiitikia dua
iliyoombwa baada ya kuzikwaMarehemu Mzee Hamid Ameir Muasisi wa
Mapinduzi,pia Mwenyekiti wa Baraza la Wazee wa CCM jana Kijijini kwao
Donge wilaya ya Kaskazini B.Unguja,[Picha na Ikulu.]
Waziri wa
nchi Ofisi ya Makamo wa Pili wa Rais Mohammed Aboud Mohammed akisoma
risala na wasifu wa Marehemu Mzee Hamid Ameir Muasisi wa Mapinduzi,pia
Mwenyekiti wa Baraza la Wazee wa CCM baada ya kuzikwa jana Kijijini
kwao Donge wilaya ya Kaskazini B.Unguja,[Picha na Ikulu.]
Maelfu
ya wananchi wakiongozwa na Rais wa Zanzibar na Mwenyeikiti wa Baraza la
Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein jana wameshiriki mazishi ya mmoja ya
waasisi wa Mapinduzi ya Zanzibar Mzee Hamid Ameir.
Mzee
Hamid Ameir ambaye alifariki jana katika hospitali kuu ya Mnazi Mmoja
mjini Zanzibar ambako alilazwa kwa matibabu amezikwa kijiji kwao Donge
wilaya Kasakazi ‘A’ Mkoa wa Kaskazini Unguja.
Kwa
mujibu wa maelezo ya serikali yaliyosomwa na Waziri wa Nchi Ofisi ya
Makamu wa Pili wa Rais Mohamed Aboud Mohamed kwa waombolezaji,marehemu
Hamid Ameir alishiriki kikamilifu katika Mapinduzi yaliyowakomboa
wananchi wa Zanzibar kutoka kwa wakoloni mwaka 1964.
Marehemu
ambaye alizaliwa 01 Januari, 1928 alijiunga na Chama cha Afro Shirazi
mwaka 1957 na kushiriki kuunda Umoja wa Vijana wa chama hicho (ASPYL).
Marehemu Hamid Ameir alishika nyadhifa mbalimbali katika serikali na Chama cha Afro Shirazi na baadae Chama cha Mapinduzi.
Aliwahi kuwa kamanda wa Jeshi la Ukombozi na pia kushika nafasi ya naibu Mkurugenzi wa Idara ya Usalama wa Taifa.
Viongozi
wengine wa kitaifa walioshiriki mazishi ya mwasisi huyo wa Mapinduzi ni
pamoja na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi na
Makamu wa Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. Mohamed
Gharib Bilal pamoja na mawaziri, makatibu wakuu na viongozi wa dini.
Kutokana
na kushiriki kwake katika Mapinduzi na kwa mchango wake katika kulinda
na kuendeleza Mapinduzi, Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la
Mapinduzi alimtunuku mzee Hamid Ameir Nishani ya Kumbukumbu ya Miaka 50
ya Mapinduzi katika sherehe zilizofanyika tarehe 11 Janauri, 2014 katika
Viwanja vya Ikulu, Zanzibar.
Mwaka huo
huo, tarehe 25 April, 2014 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk.
Jakaya Mrisho Kikwete alimtunuku mzee Hamid Ameir, Nishani ya Kumbukumbu
ya Miaka 50 ya Muungano.
0 comments:
Post a Comment