Sunday, March 6, 2016

MAZIKO YA MZEE HAMID AMEIR MUASISI WA MAPINDUZI YAFANYIKA JANA ZANZIBAR

rai1
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (katikati) pamoja na Viongozi wengine na wananchi wakibeba jeneza la Marehemu Mzee Hamid Ameir Muasisi wa Mapinduzi,pia Mwenyekiti wa Baraza la Wazee wa CCM baada ya kuswaliwa jana wakati wa Mazishi yake yaliyofanyika Kijijini kwao Donge wilaya ya Kaskazini B.Unguja,[Picha na Ikulu.]
rai2
Wananchi waliohudhuria katika mazishi ya Marehemu Mzee Hamid Ameir Muasisi wa Mapinduzi,pia Mwenyekiti wa Baraza la Wazee wa CCM wakilibeba jeneza wakati wa Mazishi yake yaliyofanyika jana Kijijini kwao Donge wilaya ya Kaskazini B.Unguja,[Picha na Ikulu.]
rai3
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (katikati) akitia udongo katika kaburi la  Marehemu Mzee Hamid Ameir Muasisi wa Mapinduzi,pia Mwenyekiti wa Baraza la Wazee wa CCM baada ya kufariki jana katika hospitali ya Mnazi Mmoja na kuzikwa  jana Kijijini kwao Donge wilaya ya Kaskazini B.Unguja,[Picha na Ikulu.]

rai4
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (katikati) pamoja na wananchi na Viongozi wakiwa katika maziko ya  Marehemu Mzee Hamid Ameir Muasisi wa Mapinduzi,pia Mwenyekiti wa Baraza la Wazee wa CCM aliyezikwa  jana Kijijini kwao Donge wilaya ya Kaskazini B.Unguja,[Picha na Ikulu.]
rai5
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (katikati) pamoja na Viongozi wengine na wananchi wakiitikia dua iliyoombwa  baada ya kuzikwaMarehemu Mzee Hamid Ameir Muasisi wa Mapinduzi,pia Mwenyekiti wa Baraza la Wazee wa CCM  jana Kijijini kwao Donge wilaya ya Kaskazini B.Unguja,[Picha na Ikulu.]
rai6
Waziri wa nchi Ofisi ya Makamo wa Pili wa Rais Mohammed Aboud Mohammed akisoma risala  na wasifu wa  Marehemu Mzee Hamid Ameir Muasisi wa Mapinduzi,pia Mwenyekiti wa Baraza la Wazee wa CCM baada ya kuzikwa jana Kijijini kwao Donge wilaya ya Kaskazini B.Unguja,[Picha na Ikulu.]

Maelfu ya wananchi wakiongozwa na Rais wa Zanzibar na Mwenyeikiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein jana wameshiriki mazishi ya mmoja ya waasisi wa Mapinduzi ya Zanzibar Mzee Hamid Ameir.

Mzee Hamid Ameir ambaye alifariki jana katika hospitali kuu ya Mnazi Mmoja mjini Zanzibar ambako alilazwa kwa matibabu amezikwa kijiji kwao Donge wilaya Kasakazi  ‘A’ Mkoa wa Kaskazini Unguja.

Kwa mujibu wa maelezo ya serikali yaliyosomwa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais Mohamed Aboud Mohamed kwa waombolezaji,marehemu Hamid Ameir alishiriki kikamilifu katika Mapinduzi yaliyowakomboa wananchi wa Zanzibar kutoka kwa wakoloni mwaka 1964.
Marehemu ambaye alizaliwa 01 Januari, 1928 alijiunga na Chama cha Afro Shirazi mwaka 1957 na kushiriki kuunda Umoja wa Vijana wa chama hicho (ASPYL).

Marehemu Hamid Ameir alishika nyadhifa mbalimbali katika serikali na Chama cha Afro Shirazi na baadae Chama cha Mapinduzi.

Aliwahi kuwa kamanda wa Jeshi la Ukombozi na pia kushika nafasi ya naibu Mkurugenzi wa Idara ya Usalama wa Taifa.

Viongozi wengine wa kitaifa walioshiriki mazishi ya mwasisi huyo wa Mapinduzi ni pamoja na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi na Makamu wa Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. Mohamed Gharib Bilal pamoja na mawaziri, makatibu wakuu na viongozi wa dini.  

Kutokana na kushiriki kwake katika Mapinduzi na kwa mchango wake katika kulinda na kuendeleza Mapinduzi, Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi alimtunuku mzee Hamid Ameir Nishani ya Kumbukumbu ya Miaka 50 ya Mapinduzi katika sherehe zilizofanyika tarehe 11 Janauri, 2014 katika Viwanja vya Ikulu, Zanzibar.

Mwaka huo huo, tarehe 25 April, 2014 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. Jakaya Mrisho Kikwete alimtunuku mzee Hamid Ameir, Nishani ya Kumbukumbu ya Miaka 50 ya Muungano.

No comments:

Post a Comment