Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete.
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete
ameamua na ameitangaza kesho, Alhamisi, Novemba 5, mwaka huu, 2015, kuwa
Sikukuu na siku ya mapumziko.
Rais
Kikwete amefanya uamuzi huo, ili kuwawezesha Watanzania kushiriki katika
sherehe za kuhitimisha Uongozi wa Serikali ya Awamu ya Nne na kuingizwa
madarakani Mheshimiwa Dkt. John Pombe Joseph Magufuli kuwa Rais wa Tano
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Kwa
mujibu wa taarifa iliyotolewa Dar es Salaam leo Jumatano, Novemba 4,
2015 na Ofisi ya Katibu Mkuu Kiongozi (KMK) Balozi Ombeni Yohana Sefue,
Rais Kikwete ametoa uamuzi huo kwa mujibu wa mamlaka aliyo nayo chini ya
Kifungu cha 3 cha Sheria ya Sikukuu za Kitaifa.
Imetolewa na:
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu,
DAR ES SALAAM.
0 comments:
Post a Comment