METDO Tanzania

METDO Tanzania

Wednesday, November 4, 2015

HAPO JANA MR CANAL NAE AITOSA MWANZA PWAAAAA

KWAHERI MWANZA...!
!....HODI DAR ES SALAAM
Ndugu zangu, Leo nimehitimisha ziara yangu ya siku 64 nikiwa Mkoani Mwanza, hakika Wakati wa uchaguzi mkuu wa Tanzania mwaka 2015 mkoa huu wa Mwanza ulikuwa na majimbo ya uchaguzi yafuatayo:
1. Buchosa : mbunge ni Dk. Charles Tizeba ( CCM )
2. Ilemela : mbunge ni Angelina Mabula (CCM )
3. Kwimba : mbunge ni Mansoor Hirani ( CCM )
4. Magu : mbunge ni Kiswaga Boniventura ( CCM )
5. Misungwi : mbunge ni Charles Kitwanga ( CCM )
6. Nyamagana : mbunge ni Stanslaus Mabula ( CCM )
7. Sengerema : mbunge ni William Ngeleja ( CCM )
8. Sumve : mbunge ni Richard Mganga Ndassa ( CCM )
9. Ukerewe : mbunge ni Joseph Mkundi (Chadema).
Katika ziara yangu hii nimetembelea Kata 167, Vijiji 5215, Mitaa 391. Huku nikifanikiwa kutembelea Kisiwa kikubwa kimoja cha Ukerewe na vingine vidogo vidogo 26.
Nikiwa Mwanza pia nimefanikiwa kuandaa mdahalo mkubwa uliofanyika kwenye ukumbi wa Mwanza Hotel kwa kuhudhuriwa na watu 497 huku Aliyekuwa mgombea ubunge Jimbo la Nyamagana Ezekiel Wenje akihudhuria zomeazomea ikamzidi akaamua kukuimbia, lakini pia mdahalo huu ulirushwa live na redio tatu zinazosikika Mkoani Mwanza na Baadhi ya mikoa ya jirani lakini pia ulirushwa na kituo bora cha luninga cha Barmedas kilichopo Mkoani hapa.
Hata hivyo pengine mdahalo huo haujawahi kufanyika nchini Tanzania kwa kufanikiwa kuwakutanisha wagombea ubunge wote wa Jimbo la Nyamagana tangu kuumbwa kwa misingi ya dunia huku mchambuzi aliyebobea katika maswala ya siasa nchini Tanzania, Humprey Polepole akiwa mgeni rasmi.
Ninaondoka Mwanza lakini bado natamani kubaki pia hakika mkoa huu una watu wakarimu sana kama watu wa Singida hakika Tanzania sote ni ndugu pasipo kujali makabila yetu.
Katika ziara yangu ya siku 64, siku 58 zote ilikuwa kila nikipost jambo mtandaoni linalohusu siasa lazima nitukanwe hakika mengi nimevumilia na zaidi matusi hayo yamenifanya kukomaa kwa kiasi kikubwa sana na kunifanya kusimamia ukweli zaidi.
Mwanza ya Sangara, Mwanza ya Sato, Mwanza ya hali ya hewa safi kabisa nitaikumbuka.
Lakini nipo safarini kuelekea Dar es salaam hakika kuna tukio kubwa ambalo isingekuwa vyema kwangu mimi kulikosa. Ni lile la kushuhudia Dkt John Pombe Magufuli Rais mteule ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania akiapishwa mbele ya watanzania.Nashukuru pia kupata mualiko huu kama vijana wengine walivyoalikwa.
Naam, kwaheri Mwanza, Hodi Dar es salaam
Wakati Mwema
Mathias Canal (Msimamia kweli)
0756413465
Gwidozebest Gwido Alex duuuu takumis my bro i hope one day we meet again
Sospeter Ndenga
Sospeter Ndenga Hongera ndugu..maana nikwaneema ya mungu tuu..
Pangani Mbiya
Pangani Mbiya karibu tena usukumani,pia waenda shuhudia msukuma akiapishwa
Like · Reply · 1 · 11 hrs
Ndimbo Ndunguru
Like · Reply · 1 · 6
Share:

0 comments:

Post a Comment

Copyright © WAZO HURU | Powered by Blogger Design by ronangelo | Blogger Theme by NewBloggerThemes.com