METDO Tanzania

METDO Tanzania

Saturday, October 10, 2015

Watu saba wauawa kwa risasi....


Burundi
Visa vya ufyatulianaji wa risasi Bujumbura vimeongezeka tangu kutekelezwa kwa jaribio la kupindua serikali miezi kadha iliyopitaWatu saba wameuawa katika mji mkuu wa Burundi, Bujumbura kufuatia kinachodaiwa kuwa jaribio la wizi katika benki moja.
Majambazi sita waliuawa na polisi baada ya gari walilotaka kutumia kutoroka kuzuiwa na polisi, polisi wamesema.
Majambazi hao walikuwa wameua afisa mmoja wa polisi awali.
Mwandishi wa BBC mjini humo Prime Ndikumagenge anasema ameona miili mitatu ikiwa katikati mwa barabara na mingine miwili katika kituo cha mafuta kilichoko karibu.
Mwili mwingine ulikuwa mita chache kutoka eneo hilo.BBC
Share:

0 comments:

Post a Comment

Copyright © 2025 WAZO HURU | Powered by Blogger Design by ronangelo | Blogger Theme by NewBloggerThemes.com