Waendesha mashtaka nchini Ufaransa wamempandisha kizimbani mwanajeshi
mmoja wa nchi hiyo kwa kosa la kuwadhalilisha kijinsia watoto wawili
wadogo wa Burkina Faso.
Duru moja ambayo jina lake halikutajwa
imeripoti kuwa, mwanajeshi huyo mwenye umri wa miaka 38 alipandishwa
kizimbani jana Ijumaa kwa kosa la kuwadhalilisha kijinsia watoto wawili
wadogo wa kike wenye umri wa miaka mitatu na mitano na kuwapiga picha za
uchi.
Mwanajeshi huyo ni kati ya wanajeshi wawili wa Ufaransa
waliosimamishwa kazi wiki hii kwa kuwadhalilisha kijinsia watoto wadogo
kwenye bwawa la kuogelea la hoteli moja nchini Burkina Faso.
Wanajeshi
hao wawili wa Ufaransa walifukuzwa nchini Burkina Faso na kurejeshwa
kwao baada ya kusailiwa na maafisa wa nchi hizo mbili huko Ouagadougou,
mji mkuu wa Burkina Faso. Wanajeshi hao ni kutoka kikosi cha jeshi la
Ufaransa kilichotumwa nchini Burkina Faso kama sehemu ya kile
kinachodaiwa ni operesheni za Ufaransa za kupambana na ugaidi. Kashfa
hiyo imekuja baada ya kashfa nyingine za udhalilishaji wa kijinsia za
wanajeshi wa Ufaransa katika Jamhuri ya Afrika ya Kati.
Saturday, July 4, 2015
KARIBU TUME YA MAENDELEO YA USHIRIKA
Popular Posts
-
📌 Asema Rais, Dkt. Samia anafanya kazi kubwa ya kuwaunganisha Watanzaia 📌 Atak...
-
Wafanyakazi wanawake wa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) Mkoa wa Dodoma, wakiwa wamejipanga tayari kwa maandamano katika maadhimisho ya S...
-
Waziri wa Kilimo Mhe Prof Adolf Mkenda akifurahia jambo pamoja na Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Marekani la Maendeleo ya Kimataifa (USAID) ...
-
Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhe. Atashasta Nditiye(wa pili kutoka kushoto) akiambatana na Msem...
Powered by Blogger.
0 comments:
Post a Comment