Saturday, July 4, 2015

Mwanajeshi wa Ufaransa adhalilisha watoto B/Faso

Waendesha mashtaka nchini Ufaransa wamempandisha kizimbani mwanajeshi mmoja wa nchi hiyo kwa kosa la kuwadhalilisha kijinsia watoto wawili wadogo wa Burkina Faso.
Duru moja ambayo jina lake halikutajwa imeripoti kuwa, mwanajeshi huyo mwenye umri wa miaka 38 alipandishwa kizimbani jana Ijumaa kwa kosa la kuwadhalilisha kijinsia watoto wawili wadogo wa kike wenye umri wa miaka mitatu na mitano na kuwapiga picha za uchi.
Mwanajeshi huyo ni kati ya wanajeshi wawili wa Ufaransa waliosimamishwa kazi wiki hii kwa kuwadhalilisha kijinsia watoto wadogo kwenye bwawa la kuogelea la hoteli moja nchini Burkina Faso.
Wanajeshi hao wawili wa Ufaransa walifukuzwa nchini Burkina Faso na kurejeshwa kwao baada ya kusailiwa na maafisa wa nchi hizo mbili huko Ouagadougou, mji mkuu wa Burkina Faso. Wanajeshi hao ni kutoka kikosi cha jeshi la Ufaransa kilichotumwa nchini Burkina Faso kama sehemu ya kile kinachodaiwa ni operesheni za Ufaransa za kupambana na ugaidi. Kashfa hiyo imekuja baada ya kashfa nyingine za udhalilishaji wa kijinsia za wanajeshi wa Ufaransa katika Jamhuri ya Afrika ya Kati.
  Mwanajeshi wa Ufaransa adhalilisha watoto B/Faso

No comments:

Post a Comment