METDO Tanzania

METDO Tanzania

Wednesday, July 15, 2015

Kifua kikuu kwa Watoto Iirnga Tatizo asilimia asilimia 15 ya wagonjwa wa kifua kikuu ni watoto.






DR Tekra Ulio Mganga mkuu wa Kifua Kikuu.

Tatizo la kifua kikuu kwa mkoa wa iringa tatizo hili limekuwa kubwa kutokana na ukosefu wa elimu ya kutosha kwa jamii huku kutokuwa na tabia ya kuwapima watoto ugonjwa wa kifua kikuu imekuwa chanzo kikuu cha ugonjwa huo kuwa zaidi kwa watoto na sababu kuu ya kuwaelemea watoto hao ugonjwa huo ni kutokana na sell za watoto hao kutostaimili uwezo wa kupambana kirusi huyo anae eneza ugonjwa huo, Zaidi anasimulia dr.Tekra Ulio ambaye ni mganga kuu wa kifua kikuu mkoa wa iringa.

Pia ametoa wito kwa jamii kuweza kuondokana na ugonjwa huo hususani kwa watoto ambao wazazi wao hupenda kushinda katika makundi ya watu wengi vilevile dalili za kuwapo kwa ugonjwa huo katika mtoto.

Aidha ametoa wito kwa jamii kuwa na utaratibu wa kuwapeleka watoto wao mara kwa mara katika vipimo kwani ugonjwa huo hutibika ikiwa haujathiri mwili zaidi tena bila gharama za matibabu yeyote.
Share:

0 comments:

Post a Comment

Copyright © WAZO HURU | Powered by Blogger Design by ronangelo | Blogger Theme by NewBloggerThemes.com