Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma, SACP David Misime
Napenda
kutoa taarifa fupi kuhusu tukio lililotokea tarehe 11/07/2015 majira ya
saa 10:00 hrs huko katika Hoteli ya St. Gasper hapa mjini Dodoma, kuwa
wananchi walitoa taarifa majira ya saa nne asubuhi kwamba kuna mtu mmoja
mwenye asili ya Kiasia amekamatwa na wananchi akiwa na fedha nyingi na
kuna vurugu kubwa.
Baada ya kupata taarifa hizo Jeshi la Polisi Mkoani hapa lilifika eneo la tukio ili kuona kama taarifa hizo ni za kweli.
Askari
walithibitisha kuwa ni kweli walimkuta mtu mmoja mwenye asili ya Kiasia
ambaye alijulikana kwa jina la AMIT KEVALRAMANI mwenye umri wa miaka 31,
Mhindi, Mfanyabiashara, Mkazi wa Dar es Salaam akiwa na fedha kiasi cha
Tshs. 722,500,000/= ambacho alipohojiwa alisema kuwa tarehe 10/07/2015
alifika Dodoma kwa ajili ya ununuzi wa mazao ya nafaka.
Alipofika
Dodoma tarehe 10/07/2015 majira ya asubuhi alifikia katika Hoteli ya
St. Gasper na tarehe 11/07/2015 aliamua kurudisha fedha benki kutokana
na kuona mkusanyiko wa watu wengi wasioeleweka na wenye viashiria vya
vurugu.
Akiwa
katika harakati ya kurejesha fedha hizo benki, ndipo kundi la watu
waliokuwa katika eneo la Hoteli ya St. GASPER walimtilia mashaka na
kumzuia asiondoke na ndipo taarifa zilitolewa polisi. Mashaka ya watu
hao yalitokana na vuguvugu za kisiasa/mchakato wa uchaguzi kati ya
makundi mbalimbali kuwa kuna watu wanahonga wajumbe. Taarifa za aina
hiyo ambazo hata Jeshi la Polisi lilikuwa limepokea bila uthibitisho.
Katika
tukio hili na uchunguzi tulioufanya tumebaini kuwa hakuna kosa la jinai
lililothibitika licha ya kukutwa na kiasi hicho cha fedha, tuhuma za
rushwa ambazo ndiyo zilikuwa msingi wa ukamataji wa mtu huyo
hazikuthibitika, kwa kuwa hakuna aliyeona akizigawa fedha hizo wala
hakuna aliyedai kushawishiwa au kugawiwa fedha hizo.
Aidha
imethibitika fedha hizo ni mali yake halali na kwa kuwa hakuna ushahidi
mwingine uliyo thibitisha vinginevyo amerejeshewa fedha zake
0 comments:
Post a Comment