METDO Tanzania

METDO Tanzania

Monday, July 20, 2015

CCM MUFINDI YAAHIDI USHINDI MNONO.

katibu wa Ccm Wilaya ya Mufindi, Jimson Mhagama alipokuwa akizungumza na wakazi wa mtaa wa Igawa.

Wananchi wa Mtaa wa Igawa Kata ya Changarawe  wilayani mufindi wakiwa katika mkutano wa chama cha mapinduzi.
katibu msaidizi wa chama cha mapinduzi wilaya ya mufindibNuru John Ngeleja akizungumza na wananchi wa mtaa Igawa.



Na Mathias Canal,

 Mufindi Ikiwa leo ni siku ya mwisho ya uchukuaji fomu kuwania nafasi ya udiwani na ubunge kwa tiketi ya chama cha mapinduzi (CCM) kinyang'anyiro ambacho kinataraji kutoa majibu na tafsiri ya nani kinara kati ya wale waliojitokeza na hatimaye kuchuana vyema na vyama vya upinzani, Chama cha Mapinduzi CCM Wilaya ya Mufindi kimeapa kushinda kwa kishindo uchaguzi mkuu kuanzia ngazi ya udiwani, Ubunge na kiti cha uwakilishi wa Taifa yaani Rais. 

 Ameyasema hayo katibu wa Ccm Wilaya ya Mufindi, Jimson Mhagama alipokuwa akizungumza na wakazi wa Mtaa wa Igawa Kata ya Changarawe Wilayani humo wakati wa mkutano wa hadhara na kuwahakikishia ushindi mnono kama ilivyokuwa kwenye uchaguzi wa serikali za mitaa. Ikumbukwe fika kwamba Chama Cha Mapinduzi CCM Wilaya ya Mufindi wakati wa Uchaguzi wa serikali za mitaa Disemba mwaka jana kilimshinda mpinzani wake ambaye ni Chama Cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA kwa tofauti kubwa ambapo katika Vitongoji 606 ccm ilishinda vitongoji 602, kwa upande wa vijiji 130 Ccm ilishinda vijiji 129 na kwa upande wa Mitaa Chadema waliambulia mtaa mmoja dhidi ya mitaa 30.

   Ushindi huo ulikipa ushindi chama cha mapinduzi Wilayani Mufindi kwa 99.9% na kupaisha mkoa wa Iringa kiliibuka kifua mbele kwa uchaguzi huo kitaifa. Mhagama alieleza kuwa ushindi huo ni tafsiri ya misingi mizuri iliyowekwa na chama hicho na watendaji wake kwa ujumla ambapo alisema kuwa ushirikiano wa viongozi wa ccm na wananchi ndiyo silaha pekee inayowatafuna na kuwaangamiza wapinzani. 
 Amesema kuwa wapinzani wana hoja dhaifu ya kukebehi maendeleo yanayofanywa na chama cha mapinduzi, wamesahau kwamba wakati nchi inapata uhuru Wilaya ya Mufindi ilikuwa na shule mbili za sekondari ambazo ni Malangali na Tosamaganga lakini hadi hivi sasa kuna shule kwa kila kata. 

 "Viongozi wa vyama vya upinzani kama vile Mbowe, Slaa na Lipumba wanapaswa kupewa shahada ya ushiriki mzuri kwenye uchaguzi mkuu bila kushinda kwenye ngazi ya Urais" Mnapaswa kutambua kwamba hivi karibuni tulikuwa Dodoma na tumewachagulia mgombea Urais ambaye anakubalika tena mchapakazi ambaye Rais Kikwete anamwita Greda huyu si mwingine ni John Pombe Magufuli hivyo tunaomba muunge mkono kwa hali na mali" Alisema Mhagama Amesema serikali ya CCM kuelekea kipindi hiki cha uchaguzi mkuu haitamvumilia mtu anayetaka kuliletea machafuko taifa kwa kuanzisha vurugu zisizo na mlengo wa kuliinua Taifa. 

 Kwa upande wake Nuru John Ngeleja ambaye ni katibu msaidizi wa Chama Cha Mapinduzi CCM Wilaya ya Mufindi amesema kuwa uchu wa madaraka ndio unautesa Umoja wa Katiba ya Wananchi (UKAWA) mpaka sasa wanashindwa kupata mgombea kwa muda mrefu sasa ilihali ccm imetumia siku mbili pekee kumpata mgombea Urais kwa kuwa ina hazina ya viongozi wa kutosha.
 Naye Makoga ambaye ni diwani aliyemaliza muda wake kwenye kata ya Isalavanu amesema kuwa ana imani kubwa atarejea tena kuiongoza kata hiyo mara baada ya kuwa ameshachukua fomu,  Sawia na hayo amewaomba wananchi hao kujitokeza kwa wingi kupiga kura kwa ccm kuanzi ngazi ya udiwani, ubunge na Rais.

Share:

0 comments:

Post a Comment

Copyright © WAZO HURU | Powered by Blogger Design by ronangelo | Blogger Theme by NewBloggerThemes.com