METDO Tanzania

METDO Tanzania

Monday, July 20, 2015

Habari picha za Dkt. John Pombe Magufuli alipopokelewa jimboni kwake

kwa chama cha Mapinduzi CCM,Dkt John Pombe Magufuli akiwasalimia wakazi wa mji huo waliojitokeza kwa wingi kumlaki,mara baada ya kuwasili jana jioni mjini humo akitokea mkoani Mwanza ambako nako alipita kujitambulisha na kuwashukuru wakazi wa jiji hilo ambao nao walijitokeza kwa wingi. Kufuatia ujio wa Dkt Magufuli ndani ya mji wa Chato kuliibuka shamra shamra za mapokezi zilizokuwa zikirindima kila pande wakifurahia uteuzi wa CCM kwa Dkt Magufuli.  Naibu Katibu Mkuu wa CCM
    Mgombea Urais kwa chama cha Mapinduzi CCM,Dkt John Pombe Magufuli akiwaaga Wananchi wa Chato waliojitokeza kwa wingi kumlaki,mara baada ya kumaliza kujitambulisha na kuwashukuru kwa kiasi kikubwa kwa kuchaguliwa kwake katika nafasi ya kupeperusha bendera ya chama chake kuwania nafasi ya Urais .   Mbunge wa Chato na Mgombea Urais kwa chama cha Mapinduzi CCM,Dkt John Pombe Magufuli akiwasalimia wakazi wa mji huo waliojitokeza kwa wingi kumlaki,mara baada ya kuwasili jana jioni mjini humo akitokea mkoani Mwanza ambako nako alipita kujitambulisha na kuwashukuru wakazi wa jiji hilo ambao nao walijitokeza kwa wingi. Kufuatia ujio wa Dkt Magufuli ndani ya mji wa Chato kuliibuka shamra shamra za mapokezi zilizokuwa zikirindima kila pande wakifurahia uteuzi wa CCM kwa Dkt Magufuli.   Baadhi ya Wananchi wa Wilaya ya Chato na vitongoji vyake waliokuwa wamekusanyika kwenye kituo cha mabasi wilayani humo wakishangilia kwa  furaha kubwa mara baada ya Mbunge wao na Mgombea Urais kwa chama cha Mapinduzi CCM,Dkt John Pombe Magufuli kujitambulisha kwao.  Baadhi ya Wananchi wa Wilaya ya Chato na vitongoji vyake wakiwa wamejitokeza kwa wingi kumlaki Mbunge wao na Mgombea Urais kwa chama cha Mapinduzi CCM, Dkt John Pombe Magufuli mara baada ya kuwasili jana jioni mjini humo na shamra shamra za mapokezi kurindima kila kona wakifurahia uteuzi wa CCM kwa Dkt Magufuli,huku wengine wakiwa wamebeba mabango kama hivyo pichani.  
Share:

0 comments:

Post a Comment

Copyright © WAZO HURU | Powered by Blogger Design by ronangelo | Blogger Theme by NewBloggerThemes.com