Wanafunzi katika shule ya Isaac Newton Academy iliyoko Ilford, Essex
nchini Uingereza wameunda mipira ya kondomu inayobadili rangi pindi
inapokutana na majimaji ya mtu anayeugua maradhi ya zinaa.
Kondomu hiyo iliyopewa jina la S.T.EYE inaweza kutambua maambukizi ya
Chlamydia Kaswende na Kisonono huku ikiwa na uwezo wa kubadili rangi
tofauti kulingana na bakteria waliopo.
Miongoni mwa wafumbuzi waliofanya uvumbuzi huu ni Daanyaal Ali (14),
Muaz Nawaz (13) na Chirag Shah (14), ambapo kufuatia ufumbuzi huo tayari
wametunukiwa, tuzo la ubunifu la ”the TeenTech” sambamba na kutunukiwa
pauni elfu moja na fursa ya kuzuru Kasri la Malkia wa Uingereza
Buckingham Palace.
Akifafanua juu ya uvumbuzi huo, mmoja wa wanafunzi hao Daanyaal Ali
amesema kuwa “Tuliazimia kumpa onyo mtumiaji wa mipira hii kuwa mpenzi
wake yuko salama ama ni mgonjwa bila ya wasiwasi wa kupimwa hospitalini
kwa ajili ya kizazi kijacho”.
Aliongeza kuwa “Swala la usalama wa mpenzi ni swala la kibinafsi kwa
hivyo ni swala linalopaswa kupewa kipaumbele haswa ikifahamika kuwa
tunawajibu wa kuchochea ngono salama bila ya kuwashurutisha wapenzi wetu
kufika hospitalini bila wao wenyewe kukusudia”
Kwa upande wake Muasisi wa kampuni ya ubunifu wa kiteknolojia,
TeenTech, Maggie Philbin alisema kuwa ni wajibu wetu kama jamii
kuchochea ubunifu unaopatikana madarasani kuchochewa na kupigwa msasa
kwa lengo la kuboresha maisha ya mwanadamu.
0 comments:
Post a Comment