METDO Tanzania

METDO Tanzania

Monday, June 22, 2015

NGUVU YA WANANCHI NI NGUVU YA MUNGU

Neno La Wakati Mwema

 


WANANCHI WAMKATAA AFISA MTENDAJI WA KIJIJI WADAI NI MWIZI

Ndugu zangu leo nimefunga safari hadi kijijini Mfyome, Kata ya Kiwele, Wilaya ya Iringa Vijijini, ni umbali wa kilomita takribani 25 kutoka makao makuu ya Mkoa wa Iringa.

Nimeshuhudia nguvu ya wananchi ikimkataa Afisa Mtendaji kisa tu wanaamini amehamishiwa pale ili kumsapoti kwenye kampeni Diwani wa Kata hiyo Paskal Mweno (CCM) ambaye wananchi hawamtaki kwa kuamini kuwa anawabeza kwenye shughuli za maendeleo.

Nimeshuhudia Afisa Mtendaji huyo Michael Mlelwa ambaye amehamishwa kutoka Kijiji cha Kiwele baada ya kupokea barua yenye kichwa kisemacho UHAMISHO na yenye kumb Na IDC/PF.123457/71 anatuhuma mbalimbali ikiwa ni pamoja na ubadhilifu wa mali hivyo wananchi wamegoma kumpokea mbele ya Afisa Mtendaji Kata ambaye ni muwakilishi wa Mkurugenzi wa Wilaya kwenye Kata na mbele ya Diwani wa kata hiyo.

Hivi karibuni Ebony Fm tuliripoti kuhusiana na tukio la Mtendaji huyo kutumia madaraka yake vibaya kwa ubabe na kubwinya pesa taarifa iliyofanyiwa uchunguzi na mwanahabari Victor Meena lakini baada ya taarifa hiyo iliyokuwa na mkazo mwingi juu ya utendaji mbovu wa kiongozi huyo hii leo tulipopata taarifa ya zawadi aliyopewa na mkurugenzi mara baada ya ubadhilifu huo ya kuhamishiwa kijiji jirani na pengine sasa taratibu zote zilishakamilika za kuanza kazi lakini wananchi wakati wa utambulisho huo tu ndipo walipotilia mkazo kumkataa wakisema kuwa hawamtaki kwa kuwa ni mwizi.

Wananchi hao walitishia kuifunga ofisi hiyo endapo tu watalazimishwa kufanya kazi na Mtendaji huyo, Kwa upande wa mwenyekiti ambaye alikuwepo awali amemwagiwa sifa nyingi na wanakijiji hao japo yeye hajaonyesha kushangazwa na uhamisho huo.

NINI NIFIKIRIACHO KWENYE HILI

Kwanza maamuzi ya Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Iringa Vijijini kumuhamisha Afisa Mtendaji huyu pasipo kuchukuliwa hatua ya kinidhamu wakati ana sifa ya wizi ni kuwakosea wananchi.

Lakini pili ni lazima wananchi na hata mimi nijenge maswali ambayo majibu yake sijui yanawezakuwaje ili nishawishike, maana Tanzania imekuwa na kasumba ya kufuga wezi wachanga kama hawa na baadaye kuwa majambazi sumbufu ambayo huvunja mabenki na uvamizi wa kutumia silaha. Yapo mambo mengi hapo yakujiuliza Je Mkurugenzi ana maslahi gani na Mtendaji kilaza kama huyu, Pengine Diwani ameshindwa vipi kumkataa kwa kuwa ana nafasi kubwa ya kukutana na wanachi kwa kuwa yeye ndiye muwakilishi wa kata hiyo kwenye vikao mbalimbali ambavyo diwani anakuwepo.

Ipo haja ya kusema sasa yatosha kwa ujinga kama huu, baada ya siku kadha utasikia tume imeundwa kufatilia kwanini wanakijiji hawamtaki huyu Mtendaji Kilaza..Yaani mkakati wa kubwinya mtonyo hapo nauona.

Hongera sana kwa wananchi ambao wamechoshwa na uzandiki kama huu
Naam, nguvu ya wananchi ni nguvu ya Mungu.If you fight against innocent person you fight against God

Ni Neno La Wakati Mwema
Mathias Canal
0756413465 canalmathias@gmail.com
Mzaliwa wa Iramba-Singida
Share:

0 comments:

Post a Comment

Copyright © WAZO HURU | Powered by Blogger Design by ronangelo | Blogger Theme by NewBloggerThemes.com