Mwenyekiti wa chama cha mapinduzi ccm Mkoa wa Iringa,Dkt.Abel Nyamahanga akipokea bendera ya chama cha ACT wazalendo kutoka kwa Ambi Daudi ambae ni Katibu wa ACT wazalendo wilaya ya Mufindi aliyejiunga na ccm leo hii katika maadhimisho ya miaka 42 ya kuzaliwa kwa chama cha Mapinduzi ccm.
Maadhimisho hayo yamefanyika kwa wilayani Mufindi kwa kushiriki katika shughuli za kijamii huku Mwenyekiti wa ccm Mkoa wa Iringa akishirikiana na Kaimu katibu wa ccm Mkoa Marco Mbaga,Mkuu wa wilaya ya Mfindi Jamhuri Davidi pamoja,Wabunge pamoja na viongozi wa ccm wilaya ya Mufindi,wanachama na wananchi,wameshiriki madhimisho hayo kwa kuchimba msingi wa ujenzi wa vyoo mbora katika shule ya sekondari Upendo,kujenga daraja,kukabidhi mifuko 49 ya saruji kwa kikundi cha vijana wajasilimali wanaojishughuliisha na utengenezaji wa tofali katika eneo la soko la Mafinga Mjini na shule ya sekondari upendo kwa ajili ya kukamilisha ujenzi wa vyoo pamoja pia wamezungumza na walimu wa wilaya ya Mufindi.
Katika maadhimisho hayo jumla ya wanachama wapya 162 wamejiunga na chama cha mapiduzi ccm,na kusema kuwa wamekunwa na utendaji mzuri wa Rais Magufuli.
(PICHA NA ESTA MALIBICHE)
Mwenyekiti wa ccm Mkoa wa Iringa Dkt. Abel Nyamahanga akivarishwa skuf mara baada ya kuwasili katika ofisi za ccm wilaya ya Mufindi leo asubuhi.
0 comments:
Post a Comment