Serikali
ya Afrika Kusini imekana ripoti kwamba mawaziri wake walipanga njama ya
kumtorosha rais wa Sudan Omar El Bashir wiki iliopita.
Nusra
rais huyo akamatwe kufuatia agizo la mahakama ya kimataifa kuhusu
uhalifu wa kivita dhidi yake kutokana na mashtaka ya mauaji ya kimbari.
Mahakama ya Afrika Kusini ilimuagiza Bashir kusalia nchini humo huku ikijadiliana kuhusu iwapo agizo hilo litekelezwe.
Lakini kabla ya mahakama hiyo kutoa uamuzi wake bwana Bashir aliondoka nchini Afrika Kusini na kurudi nyumbani.
Rais huyo
wa Sudan alikuwa nchini Afrika Kusini kwa mkutano wa viongozi wa bara
Afrika na kwamba serikali ilikuwa inajua kwamba ilihitajika kumkamata
kwa kuwa mwanachama wa ICC.
Lakini
gazeti la Sunday Times nchini Afrika Kusini limenukuu duru za serikali
kwamba katika mkutano wa mawaziri ilikubalika kwamba Afrika Kusini
itamlinda hata iwapo italazimika kukiuka uamuzi wa mahakama na kukiuka
katiba.
Katika
taarifa ,serikali imekana kwamba kulikuwa na mkutano wa siri na kwamba
itaipatia mahakama hiyo maelezo kuhusu vile Bashir alivyoondoka nchini
humo.
Mahakama kuu imeipatia serikali ya taifa hilo hadi alhamisi kubaini ni vipi aliruhusiwa kuondoka.
CREDIT: BBC SWAHILI
0 comments:
Post a Comment