METDO Tanzania

METDO Tanzania

Monday, February 5, 2024

SETIKALI KUKARABATI SKIMU YA UMWAGILIAJI YA MASENGWA-SHINYANGA

SERIKALI imesema kuwa Skimu ya Masengwa iliyopo kata ya Masengwa Wilaya ya Shinyanga Vijijini, Mkoani Shinyanga inachangia kwa kiasi kikubwa uzalishaji wa zao la mpunga na mbogamboga kupitia kilimo cha umwagiliaji. 

Hayo yameelezwa Bungeni Jijini Dodoma na Naibu Waziri Wa kilimo David Silinde alipokuwa akijibu swali la Mbunge wa Viti Maalum Dkt. Christina Mnzava alipouluza Je, ni kuna mpango gani wa kukarabati skimu ya umwagiliaji ya Masengwa-Shinyanga?

"Mheshimiwa Spika, Ninapenda kujibu swali la Mheshimiwa DKT. CHRISTINA CHRISTOPHER MNZAVA, Mbunge wa Viti Maalum kama ifuatavyo, 

Mheshimiwa Spika, Skimu hii ina uwezo wa kumwagilia hekta 540, kutokana na uchakavu wa mfereji mkuu wa skimu hiyo eneo linalomwagiliwa kwa sasa ni hekta 133,"alisema Naibu Waziri. 

Aidha, alisema kuwa Tume ya Taifa ya Umwagiliaji kupitia wataalamu wake wa ndani waliopo katika ngazi ya Wilaya na Mkoa wanaendelea na kazi ya kubaini mahitaji halisi ya ukarabati wa skimu hii ili iweze kuwekwa katika mpango wa bajeti ya mwaka 2024/2025.
Share:

0 comments:

Post a Comment

Copyright © WAZO HURU | Powered by Blogger Design by ronangelo | Blogger Theme by NewBloggerThemes.com