METDO Tanzania

METDO Tanzania

Monday, February 5, 2024

SERIKALI KUINGIZA VITUO VYA AFYA KWENYE MFUMO WA KUSAMBAZA DAWA KWA KUTUMIA DRONE


SERIKALI ipo kwenye hatua ya kuingiza vituo vyote ya afya kuanzia zahanati hadi Taifa kwenye mfumo wa kusambaza dawa kwa kutumia ndege maalumu (drones) kwa ajili ya kuufanyia majaribio.

Hayo yamesemwa bungeni leo na Naibu Waziri wa Afya, Dk. Godwin Mollel wakati akijibu swali la Mbunge wa Kilindi, Omary Kigua(CCM)

Katika swali lake, Mbunge huyo ametaka kujua ni lini serikali itatumia Drones kusambaza Dawa katika Zahanati za vijijini.

Akijibu swali hilo, Mollel amesema ilikamilisha mfumo ambao unahifadhi taarifa zote za vituo kuanzia ngazi ya Zahanati hadi Taifa.

“Mfumo huu utasaidia kupata taarifa za kijiografia za vituo vyote nchini,”amesisitiza Dk. Mollel.

Ameongeza kuwa :“Sasa tupo kwenye hatua ya kuingiza vituo vyote kwenye mfumo huu ili kuufanyia majaribio na pia kutazama gharama za usafirishaji dawa kupitia mfumo huo wa ndege maalum (drones) ukilinganisha na usafirishaji kwa njia ya magari ili maamuzi sahihi yafanyike”.
Share:

0 comments:

Post a Comment

Copyright © WAZO HURU | Powered by Blogger Design by ronangelo | Blogger Theme by NewBloggerThemes.com