METDO Tanzania

METDO Tanzania

Monday, July 3, 2023

MWENYEKITI UVCCM IKUNGI ZULFAT MUJA AWATAKA VIJANA KUENDELEA KUUNGA MKONO JUHUDI ZA SERIKALI

Mwenyekiti wa UVCCM wilaya ya Ikungi bi Zulfat Muja jana tarehe 02.07.2023 alifunga Ligi ya mpira wa miguu iliyokuwa inaendelea kata ya Puma.

Bi Zulfat Muja ambaye pia alikuwa mgeni rasmi katika mashindano hayo aliwasihi vijana kuendelea kukiunga mkono Chama cha Mapinduzi na serikali inayoiongoza chini ya Mwenyekiti na Rais Dkt Samia Suluhu Hassan.

"Serikali yenu ya Chama cha Mapinduzi inatambua umuhimu wa vijana katika ujenzi wa nchi, Na ndio maana asilimia zaidi ya vijana waliteuliwa kuwa wakurugenzi na makatibu tawala katika wilaya na halmashauri mbalimbali hapa nchini" Alisema Muja.

Katika kuhitimisha Ligi hiyo Bi Muja alikabidhi zawadi mbalimbali kwa washindi ili kuendelea kuhamasisha ushiriki wa vijana katika Michezo, Ambapo bingwa alinyakulia Tsh 300,000, Mshindi wa pili alijikusanyia Tsh 150,000, Na mshindi wa tatu akikusanya kitita cha Tsh 75,000 kutoka kwa mgeni rasmi.
Share:

0 comments:

Post a Comment

Copyright © WAZO HURU | Powered by Blogger Design by ronangelo | Blogger Theme by NewBloggerThemes.com