Rais Wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania *Dr John Pombe Joseph Magufuli* ameiagiza Wizara ya Fedha kushirikiana na Taasisi mbalimbali ikiwemo Bunge ili kutatua changamoto ya kodi inayotozwa katika mchuzi wa zabibu ambayo imepelekea kuongezeka kwa gharama za uzalishaji wa Mvinyo(**wine**) ikilinganishwa na mvinyo unaotoka nje ya nchi na hivyo kuwafanya wakulima wa zabibu kukosa soko la uhakika.
Mh Rais ametoa maagizo hayo leo katika hafla ya Ufunguzi wa Jengo jipya la PSPF Plaza na Tawi la NMB la Kambarage ambapo alikuwa akijibu maombi ya Mbunge wa Dodoma Mjini *Mh Anthony Peter Mavunde* ambaye pia ni Naibu Waziri wa Kazi,Vijana na Ajira aliyemuomba Mh Rais kusaidia kutatua changamoto hiyo kodi ya mchuzi wa zabibu ambao imefikia **Tsh 3315 **kwa lita na hivyo kuwafanya wanunuzi wakubwa kushindwa kuchukua mchuzi kutoka katika Viwanda vya Dodoma ambao nao wameshindwa kununua zabibu kutoka kwa Wakulima kwa kukosa soko la uhakika la mchuzi huo hali iliyopelekea zaidi ya *tani 300* za zabibu kuozea shambani na kusababisha hasara kubwa kwa Wakulima.
Agizo hilo limepokelewa kwa furaha kubwa na Wakulima wa zabibu wa mkoa wa Dodoma ambao wanategemea zao la zabibu kuendesha maisha yao ya kila siku kwa kuwa tatizo hilo likishughulikiwa watapata uhakika wa soko la mazao yao tofauti na ilivyo hivi sasa.
0 comments:
Post a Comment