Na Saida Issa,Dodoma
MBUNGE wa Geita vijijini Joseph Musukuma amewataka watanzania kutoyumbwisha na maneno ya watu wasioitakia mema Nchi bali waunge mkono judihada za Rais kwenye Uwekezaji wa bandari ya Dar es salaam ambao utakuwa na tija kwa wafanyabiashara.
Mbunge huyo ameyasema hayo jijini Dodoma wakati akizungumza na waandishi wa habari baada ya kuwepo kwa maneno kwenye mitandao ya kijamii ambapo baadhi ya watu wamekuwa wakisema bandari hiyo imeuzwa na wengine wakisema mkataba wa miaka 100.
"Tuache kudanganyana Mimi nimefika Dubai nimejionea namna bandari za wenzetu zinavyofanya kazi, Uwekezaji unaofanywa na Serikali yetu inayoongozwa na Rais Samia utasaidia sisi wafanyabiashara malalamiko ya kucheleweshewa mizigo bandarini"alisema Musukuma.
Alisema kuwa hali iliyopo Kwa sasa bandarini katika upokeaji wa mizigo unachukua muda mrefu na inapelekea wafanyabiashara wengi kuagiza mizigo kupitia bandari nyingine ikiwemo bandari ya Mombasa.
"Taasisi ya Rais inawatu wengi sio kwamba wanavyozungumza mitandaoni hakuna tafiti zilizofanyika,Ikulu imefanya utafiti na sisi wabunge baadhi tulienda kuona na kuona ni kuamini,na sio wanaozungumza mitandaoni wanauwezo mkubwa Sana sio kweli unaweza uakawa na uwezo mukubwa wa kuzungumza Mitandaoni lakini hujui mateso yaliyopo bandarini ukabaki tu kushindwa mitandaoni,kujadili wenzio na kupiga vitu ambavyo huna uhakika navyo,"alisema Msukuma.
Kadhalika aliwataka watanzania kuunga mkono azimio hilo na kama kunamapunguvu yatasimama kwenye mkataba kwani Kwa sasa kinachojadiliwani makubaliano ya Nchi na Nchi.
"Mimi naamini maneno yanayoandikwa kwenye Mitandao sio ya kweli kwasababu hata Rais Samia atastaafu na yeye ataishi maisha kama ya kwetu si kweli kama ataenda kusaini mkataba ambao hauna maslahi kwa Taifa hili labda yeye kama iwe akistaafu anahama Tanzania lakini hapana tusikatishane tamaa,
Turudi nyuma watanzania hakuna mkataba wa kimkakati ambao tumeufanya kwenye awamu zote bila kuwa na kelele na kelele hizi zinatengenezwa na watu wasiiitakia mema Nchi yetu,"alisema Msukuma.
0 comments:
Post a Comment