Na Saida Issa, Dodoma
SERIKALI imesema kamati ya Taifa ya kupanga barabara katika hadhi stahiki NRCC ilifanyika mkoani Mbeya februari 24 mwaka huu na kutembelea barabara zilizoombwa kupandishwa hadhi ikiwemo barabara ya Irambo- msonyanga.
Hayo yameelezwa Bungeni Jijini Dodoma na Naibu Waziri wa TAMISEMI Deogratus Ndejembi alipokuwa akijibu swali la Mbunge wa Mbeya Vijijini Oran Njeza.
Ndejembi alisa kuwa mapendekezo ya kamati yaliwasilishwa kwa Waziri wa ujenzi na uchukuzi na yanachambuliwa na uchambuzi ukikamilika taarifa itatolewa endapo barabara hiyo itakidhi vigezo vya kupamdishwa hadhi itakuwa barabara ya mkoa na itahudumiwa na wakala wa barabara Tanzania TANROAD.
Mbunge Njeza alisema kuwa Waziri wa Ujenzi ameridhia barabara hiyo kuwa ya mkoa lakini ipo katika hali mbaya sana na je, ni lini Serikali itaanza Ujenzi wa barabara hiyo ili ianze kupitika na barabara ya ilembwe- Isonso ambayo inaunganisha mbeya na mkoa wa Songwe je,ni lini nayo itapandishwa hadhi kuwa ya mkoa?
Naibu Waziri alisema kuwa barabara ikiwa imeshakidhi kwenye vigezo vya kupamdishwa hadhi na ikapandishwa hadhi na ikawa inahudumiwa na TANROAD basi ni wajibu wa TANROAD kutenga bajeti hiyo na kuweza kutengeneza barabara.
"Tutakaa na wenzetu wa Wizara ya Ujenzi na kuona wao wamejipanga vipi kwaajili ya kutengeneza barabara hii ambayo ni muhimu sana kule Jimboni Kwa Mheshimiwa Njeza,"amesema.
Pia amesema kuwa barabara ya Irembo-Isonzo ambayo inaunganisha wilaya ya mbeya na Wilaya ya Songwe lakini hasa katika wilaya ya ileje
"Barabara hii itapandishwa hadhi pale ambapo watafata vigezo vya kisheria kama ambavyo barabara nyingine zinafanya waanze vikao vyao katika DCC waende kwenye RCC na baadae Bodi ya barabara ya mkoa na kisha kumuandikia Mheshimiwa Waziri wa Ujenzi na uchukuzi mwenye dhamana ya barabara hizi za mkoa ili team iweze kutumwa kwenda kwenye barabara hii ya ilembwe- naIsonzo kufanya tathmini na kisha kumshairi Waziri wa Ujenzi kuhusu barabara hizi kupamdishwa hadhi,"amesema Ndejembi.
0 comments:
Post a Comment