Mkuu wa Mkoa wa Singida Peter Serukamba akizungumza na wananchi wa Kijiji cha Masagi Kata ya Mtoa Wilayani Iramba wakati akisikiliza kero leo Mei 2, 2023. |
Mkuu Wa Wilaya ya Iramba Suleiman Mwenda Akifafanua jambo wakati Mkutano wa Mkuu wa Mkoa wa kusikiliza kero katika Kijiji cha Masagi Wilayani Humo. |
Wananchi wa Kijiji cha Masagi wakifuatilia hoja mbalimbali kwenye Mkutano huo. |
Na, Hamis Hussein – Iramba, Singida
MKUU wa Mkoa wa
Singida Peter Serukamba amepiga marufuku shughuli za kibinadamu ikiwemo kulima,
kuchungia mifugo na kuanzisha ujenzi wa makazi katika hifadhi ya Msitu wa
Sekenke uliopo Wilaya ya Iramba ili kulinda msitu huo utakaosaidia kukabiliana
na mabadiliko ya tabia ya nchi.
RC Serukamba
amesema hayo leo Mei 2, 2023 wakati akisikiliza kero za wananchi wa Kijiji cha
Masagi kata ya Mtoa Wilayani Iramba ambapo wananchi waliiomba serikali ya
Wilaya kuwaruhusu kuchungia mifugo yao kwenye Hifadhi ya Msitu huu.
Mkuu huyo
amesema kuwa shughuli za kibinadamu kwenye hifadhi za misitu ndio sababu ya
kupelekea ukame ambao umekuwa ukiathiri shughuli za uzalishaji kama vile kilimo
hivyo amewataka wananchi hao kuanza kutenga Maeneo ya malisho pamoja na
kuanzisha kilimo cha Nyasi kwaajili ya Kulisha Mifugo yao.
“Wazee nyie mmekuwa hapa kote huko kulikuwa
na misitu kwasababu wazazi wetu waliinda misitu haiwezekani sisi tuache kulinda
misitu Mlima Sekenke lazima tuulinde, Habari ya kuchunga, Kukata kuni huko
haipo, umefika wakati mtu awe anatenga eneo la kufugia na ardhi ambayo utalima,
tubadilike muanze kuwa na maeneo ambayo mtakuwa mnalima nyasi za kulisha
mifungu sasa hivi Dunia Imefikia huko”
Alisema RC Serukamba
Kwa upande wake
Mkuu wa Wilaya ya Iramba Suleiman Yusuph Mwenda amesema kuwa kuharibiwa kwa
misitu katika kata ya Mtoa na Maeneo mengine kumepelekea kuharibu vyanzo vya
maji na mvua hali ambayo imeathiri uzalishaji ukilinganisha na hapo awali
ambapo kulikuwa na misitu mingi ambayo ilikuwa inavutia mvua.
DC Mwenda Aliongeza
kuwa awali Wilaya ya Iramba ndio ilikuwa eneo pekee lenye vyanzo vingi vya maji
kwa kuwa na Maziwa na mabwawa ikiwemo ziwa Kitangiri, Doromoni, Mabwawa ya
Urughu na Mayanzani lakini kwa sasa kutokana na uharibifu wa misitu vyanzo
hivyo vimeathirika na vingine kukauka.
Kero Nyingine
iliyowasilishwa na wananchi wa Masagi ni katika idara ya afya ambapo wananchi
wa Kijiji hicho walimueleza Mkuu wa Mkoa kuwa wahudumu wa afya wamekuwa hawatoi
huduma nzuri kwa wananchi hasa akina mama wakati wa kujifungua na kupelekea
kujifungulia nyumbani.
Kufuatia Kero
hiyo RC Serukamba amemwagiza Mganga Mkuu wa Mkoa wa Singida kuanza kuwafuatia
wataalam na wahudumu wa afya ngazi za Chini ili kuhakikisha huduma nzuri
zinatolewa kwa wananchi.
Pamoja na Mambo
mengine Rc Serukamba amemwagiza Mganga Mkuu wa Wilaya ya Iramba kumalizia hatua
zilizo bakia kwenye Zahanati ya Kijiji cha Masagi ambapo ametoa siku tano
zahanati hiyo ianze kutoa huduma kwa wananchi.
0 comments:
Post a Comment