METDO Tanzania

METDO Tanzania

Thursday, May 4, 2023

MBUNGE KASSINGE AIOMBA SERIKALI KUJENGA BWALO KATIKA CHUO CHA MASOKO KILWA

Na Saida Issa, Dodoma

MBUNGE wa kilwa kusini Ally Kassinge ametaka kujua nilini Serikali itawapatia fedha za Ujenzi wa bwalo katika Chuo Cha kilwa masoko kwani miundombinu yake imechakaa.

Ameeleza Bungeni Jijini Dodoma ambapo ametaka kujua Serikali itawapatia fedha hizo lini kwani miundombinu ya Chuo Cha masoko imekuwa chakavu na kwasasa kipaumbele chake ni kujenga bwalo katika chuo hicho.

Akijibu swali hilo la nyongeza Naibu Waziri wa Wizara ya Elimu,Sayansi na Teknolojia Omary Kipanga amesema kuwa Mpango wa Serikali ni Ujenzi wa vyuo 64 katika wilaya ambazo hazina na miongoni mwa wilaya hizo ni pamoja na Wilaya ya kilwa.

"Tunatambua uwepo wa Chuo Cha masoko pale kilwa kusini na tunajua kwamba kinauhitaji wa bwalo pamoja na baadhi ya mabweni hivyo Katika mwaka wa fedha ujao tutatenga fedha kwaajili ya ukarabati wa vyuo hivyo ikiwemo mabweni pamoja na bwalo,"amesema Naibu Waziri.
Share:

0 comments:

Post a Comment

Copyright © WAZO HURU | Powered by Blogger Design by ronangelo | Blogger Theme by NewBloggerThemes.com