METDO Tanzania

METDO Tanzania

Tuesday, May 2, 2023

WAZIRI MKUU AIPONGEZA KAMPUNI YA ASAS KWA HUDUMA WANAYOITOA KWA JAMII

Na Saida Issa, Dodoma

WAZIRI Mkuu Kassim Majaliwa ameridhishwa na maonesho yaliyoandaliwa na Wizara ya Mifugo na uvuvi yaliyopo katika viwanja vya Bunge huku akiwapongea ASAS kwa huduma wanayoitoa kwa jamii.

Waziri Mkuu ameyaeleza hayo alipotembelea mabanda hayo yaliyopo katika viwanja vya Bunge na kuwataka ASAS waendelee kuhudumia jamii kwa kuzalisha maziwa mengi na Bora.

Aidha amemuagiza Waziri wa Mifugo na uvuvi kuwa kampuni kama ASAS na nyinginezo waangalie namna ya kuweza kuzisaidia kwani zinafanya kazi kubwa ya kuzalisha bidhaa ambazo zinaweza kuuzika hata nje ya Nchi.

"Wizara imeonyesha mikakati wa namna inavoboresha sekta ya Mifugo na uvuvi,namna Serikali inayoongozwa na Dkt.Samia Suluhu Hassan kwa kuridhia kutenga fedha ya kutosha kwa sekta mbili na tumeweza kupata mafanikio na tumeona changamoto zilizojitokeza huko nyuma,

Tukiwa tunaendelea na mawasilisho yetu ipo fursa ya wabunge kuchangia kwa sekta hizi mbili za Mifugo na uvuvi kwa kuchangia maoni ya wananchi wanavyoeleza na pia wanatoa muelekeo wa Nini Wizara ifanye,"amesema Waziri Mkuu.

Kwa upande wake Waziri wa Mifugo na uvuvi Abdallah Ulega amesema kuwa watahakikisha wanashirikia na ASAS kuhakikisha wanapata maziwa ya kutosha ili kupunguza uaguzaji wa maziwa ya unga.

"watanzania tumepiga hatua kwani Mifugo na uvuvi ni utajiri unaweza kuinua Pato la Nchi na uchumi wa mtu mmoja mmoja,

Tunakila sababu ya kujivunia hili na kuendelea kuongeza kasi katika kuitunza Mifugo yetu ili tuendeleze kuzalisha Mifugo mingi na Bora zaidi,"amesema.

Naye Mkurugenzi Mtendaji wa ASAS Fuad Asas amesema Wizara ya Mifugo na uvuvi imewapa ushirikiano hasa katika kusaidia uzalishaji wa maziwa na upatikanaji wa ng'ombe Bora kwa kuwaunganisha na wafugaji wa ng'ombe Bora.

Kadhalika alisema kuwa ipo haja ya Wizara ya Mifugo kuhakikisha inatoa elimu ya kutosha kwa wafugaji ili kuepusha matatizo yatokanayo na maziwa kutoka kwa ng'ombe kwenda Kwa mlaji.

Balozi wa ASAS Lucas mhuvile amesama kuwa lengo kuu ni kuhakikisha jamii kwa ujumla inapata elimu ikiwa sambamba na kutumia maziwa kwa wingi ili kuimarisha na kuboresha afya zao.
Share:

0 comments:

Post a Comment

Copyright © WAZO HURU | Powered by Blogger Design by ronangelo | Blogger Theme by NewBloggerThemes.com