METDO Tanzania

METDO Tanzania

Tuesday, May 9, 2023

MBUNGE USSI ATAKA KUJUA HATUA ILIYOBAKI KATIKA MCHAKATO WA KUPATA KATIBA MPYA

Na Saida Issa, Dodoma

SERIKALI imesema imejipanga kutoa elimu ya Katiba iliyopo ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 77 pamoja na katiba ya Zanzibar ya mwaka 84 Kwa kuhakikisha wananchi wanapata elimu ili wazifahamu kabla mchakato wa Katiba mpya haujaendelea.

Hayo yameelezwa na Naibu wa katiba na sheria Pouline Gekulu alipokuwa akijibu swali la lililoulizwa kwa niaba ya Mbunge wa Chumbuni Ussi Salum Pondeza kuwa Je, ni lini hatua iliyobakia katika mchakato wa kupata Katiba Mpya itakamilishwa baada ya kupitishwa.

Alisema kuwa wananchi wote watashurikishwa katika mchakato wa Katiba mpya na watapata nafasi ya kutoa maoni.

"Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kutambua umuhimu wa mchakato wa kupata katiba mpya aliunda kikosi kazi kilichoongozwa na Prof. Mukandara ambacho Pamoja na masuala mengine ilikua ni kuhuhisha mchakato wa katiba mpya na katika hilo, kikosi kazi hicho kimetoa mapendekezo ya hatua sita (6) za kufuatwa katika kukamilisha mchakato wa kupata Katiba Mpya,"alisema Naibu Waziri.

Alisema kuwa Hatua hizo ni; kuwepo kwa Mjadala wa Kitaifa wa kupata muafaka wa masuala ya msingi, kuhuisha Sheria ya Mabadiliko ya Katiba, Kuundwa kwa Jopo la Wataalam wa kuandaa Rasimu ya Katiba,Rasimu ya Katiba kupitishwa na Bunge,Kutoa elimu ya uraia na hatua ya mwisho ni Rasimu ya Katiba kupigiwa kura na Wananchi.

"Baada mapendekezo ya kikosi kazi, tarehe 06 Mei, 2023 Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassani, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania alimuagiza Msajili wa Vyama vya Siasa kuitisha Kikao Maalum cha Baraza la Vyama vya Siasa kujadili mapendekezo ya kikosi kazi na kupendekeza taratibu za kuzingatia katika kuanzisha mchakato wa kupata Katiba Mpya,"alisema.
Share:

0 comments:

Post a Comment

Copyright © WAZO HURU | Powered by Blogger Design by ronangelo | Blogger Theme by NewBloggerThemes.com