METDO Tanzania

METDO Tanzania

Wednesday, May 10, 2023

MBUNGE ORANI AIPONGEZA BAJETI YA KILIMO KUWA NI NGUZO KUU YA UCHUMI WA TANZANIA


Na Saida Issa, Dodoma

MBUNGE wa Mbeya Vijijini Oran Njeza ameishukuru Wizara ya Kilimo kwa kutoa mapendekezo mazuri yanayoonesha kuwa Kilimo kwa sasa kinaweza kuwa ni nguzo kuu ya Uchumi wa Tanzania.

Mbungu huyo ameyasema hayo katika viwanja vya Bunge Jijini Dodoma amesama kuwa Kwa sasa Kilimo kinaonesha kuwa kinaweza kuwa ndio nguzo kuu ya Uchumi wa Tanzania Kutokana na mapendekezo yaliyotolewa kupitia bajeti ya mwaka wa fedha 2023/24.

Amesema kuwa bajeti hiyo umeweka mkazo katika Kilimo Cha umwagiliaji pamoja na masoko kwani hicho ndicho kilikuwa kilio kikubwa kwa wakulima.

"Mwenyezimungu amemjaaliwa Mheshimiwa Rais Kwa vile alivyotoa kwanza ruzuku ambayo mabilioni mengi ya fedha ameyatoa kwenye ruzuku na Kwa mwaka huu tumeona mabadiliko hasa ya mazao kwenye halmashauri yangu kwani wakulima wamefaidi sana na tunategemea mazao yatakuwa mazuri na Kilimo kimeonesha tija,"amesema.

Pia amesema kuwa Muhimu suala la masoko liangaliwe kabla mkulima hajalima sio mkulima alime baadae apate changamoto ya masoko.

"Dunia ya Leo inataka tuende na jinsi ambavyo inaenda hapa namshauri Waziri wa Kilimo aangalie kwa makini na kumsaidia mkulima pale anapokuwa amekamilisha shughuli zake za Kilimo basi asihangaike kutafuta masoko,"amesema.
Share:

0 comments:

Post a Comment

Copyright © WAZO HURU | Powered by Blogger Design by ronangelo | Blogger Theme by NewBloggerThemes.com