METDO Tanzania

METDO Tanzania

Wednesday, May 24, 2023

MBUNGE NJEZA AIOMBA SERIKALI KUKAMILISHA BARABARA.


Na Saida Issa, Dodoma

MBUNGE wa Mbeya Vijijini Oran Njeza ameiomba Serikali kuhakikisha inakamilisha barabara ambazo ni kiunganishi kikubwa kwa nchi zinazoizunguka Tanzania ikiwemo Malawi pamoja ma Zambia pamoja na kulisha uwanja wa ndege.

Mbunge huyo ameyasema hayo alipokuwa akichangia katika bajeti ya Ujenzi na Uchukuzi Bungeni Jijini Dodoma amesema barabara hizo ni pamoja na Isionje,kikondo makete kuwa ni barabara muhimu sana.

"Mheshimiwa waziri hebu chukulia hiyo umuhimu wa kipekee na kuipa kipaumbele ili iweze kujengwa haraka kwasababu uchumi wa mikoa yetu njombe,mbeya,ruvuma na Iringa inategemea zaidi usafirishaji wa mizigo ili iweze kubebwa na kupelekwa nje na Tanzania iweze kupata pesa za kigeni,

Lakini barabara nyingine ambayo ni muhimu Mheshimiwa Waziri ni barabara ya Mbarizi,chang'ombe mkwajuni kwenda mpaka makongolosi kwa umuhimu wake hii barabara ni ahadi ya muda mrefu sana lakini imekuwa haipewi umuhimu nakuomba sana katika bajeti hii hii barabara ipewe kipaumbele Cha pekee iweze kujengwa kwa Kiwango cha Rami,"amesema.

Aidha amesema kuwa Nchi ya Tanzania imepewa neema ya kuwa na geographia nzuri Kwa kuwa na bandari,maziwa lakini bado havijatumiwa vizuri kwani bandari ya dar es salaam ufanisi wake bado haujatumiwa vizuri ukilinganisha na bandari zingine.

"Ufanisi wake ukilinganisha na bandari nyingine sisi inawezekana ni wapili kutoka wa mwisho na wa mwisho nafikiri ni Somalia sasa hatuwezi kuanza kujilinganisha namna hiyo tuchukue hatua za haraka ili tuboreshe ufanisi wa bandari yetu,"amesema Mbunge huyo.
Share:

0 comments:

Post a Comment

Copyright © WAZO HURU | Powered by Blogger Design by ronangelo | Blogger Theme by NewBloggerThemes.com