METDO Tanzania

METDO Tanzania

Wednesday, May 24, 2023

JE?SERIKALI INAMPANGO GANI WA KUTOA MWONGOZO KWA WAWEKEZAJI ILI KUCHANGIA SHUGHULI ZA MAENDELEO YA JAMII KATIKA MAENEO WANAYOWEKEZA?"MBUNGE MWAKAMO"


Na Saida Issa, Dodoma

SERIKALI imesema kuwa iliandaa Mwongozo wa Taifa wa Ushiriki wa Watanzania katika Sekta mbalimbali wa mwaka 2019 yaani “National Multsector Local Content Guideline” kwa ajili ya kusimamia masuala ya ushiriki wa Watanzania katika Miradi ya Kimkakati na Uwekezaji. 

Hayo yameelezwa Bungeni Jijini Dodoma na Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara Exaud Kigahe alipokuwa akijibu swali la Michael Costantino Mwakamo, Mbunge wa Jimbo la Kibaha Vijijini alipouliza Je, Serikali ina mpango gani wa kutoa Mwongozo kwa wawekezaji ili kuchangia shughuli za maendeleo ya jamii katika maeneo wanayowekeza?

"Mheshimiwa Spika, katika kuhakikisha Wawekezaji wanachangia shughuli za 
maendeleo za jamii katika maeneo wanayowekeza, Serikali ina sheria za kisekta na miongozo inayosimamia Wawekezaji katika Sekta ya Uziduaji ambayo ni Mwongozo wa Ushiriki wa Watanzania katika Sekta Ndogo ya Mafuta 2019;

Mwongozo wa Kuwasilisha Mpango wa Ushiriki wa Watanzania katika Sekta ya 
Madini wa mwaka 2018 na Mwongozo kwa Mamlaka za Serikali za Mitaa kuhusu Uwajibikaji kwa Jamii wa Makampuni wa mwaka 2022,"amesema Naibu Waziri.

Pia amesema kuwa Utaratibu huo unaruhusu wawekezaji kuchangia sehemu ya mapato yake kwa jamii ikiwa ni sehemu ya uwajibikaji kwa jamii na kuchangia shughuli za maendeleo katika eneo la uwekezaji kupitia Mamlaka za Serikali za Mitaa.
Share:

0 comments:

Post a Comment

Copyright © WAZO HURU | Powered by Blogger Design by ronangelo | Blogger Theme by NewBloggerThemes.com