METDO Tanzania

METDO Tanzania

Tuesday, May 16, 2023

KOMRED KHERI JAMES AHIMIZA UMAKINI ZAIDI KATIKA USIMAMIZI WA MIRADI.









Mkuu wa wilaya ya Mbulu Komred Kheri James mapema Leo amewataka wahandisi na Idara ya ujenzi kwa ujumla kuongeza umakini katika usimamizi wa miradi,ili  kuhakikisha thamani ya fedha na ubora wa miradi vinazingatiwa,ili kukamilisha miradi kwa wakati,na kutoa huduma kwa ufanisi unatarajiwa na Wananchi.                      

Komred Kheri James ameyatoa maelekezo hayo mapema leo katika Ziara ya Ukaguzi wa Miradi katika Halimashauri ya Mji wa Mbulu, ikiwa ni Sehemu ya Maandalizi ya Mapokezi ya Mbio za Mwenge Wilayani Mbulu.                       

Pamoja na Mambo Mengine, Komred Kheri James amewasihi Viongozi wa kila Ngazi Kutenga Muda wa Kujua,

na Kufatilia Miradi inayotekelezwa katika Maeneo yao na Kutoa Taarifa kwa Wananchi, na Mamlaka zinazo husika endapo watabaini Dosari ili hatua zichukuliwe kwa wakati.                                     

Ukaguzi wa Miradi katika Halimashauri ya Mbulu Mji imehusisha miradi nane ya Afya, Elimu, Kilimo, Maji, Uhifadhi wa vyanzo vya maji, na Miundombinu. Ziara hii imehusisha Wajumbe wa Kamati ya Usalama, Mkurugenzi wa Halimashauri ya Mbulu Mji na Wataalamu.                 

Mwenge wa Uhuru Unatarajiwa Kupokelewa Halimashauri ya Mbulu Mji Tarehe 12 October 2023.                                       


#KwaPamoja,Tunaijenga Mbulu Yetu

Share:

0 comments:

Post a Comment

Copyright © WAZO HURU | Powered by Blogger Design by ronangelo | Blogger Theme by NewBloggerThemes.com