METDO Tanzania

METDO Tanzania

Friday, May 5, 2023

Kero za Huduma za Jamii, Ardhi Mnang'ana Ikungi zatatuliwa











Na Hamis Hussein - Ikungi, Singida

MKUU wa Mkoa wa Singida Peter Serukamba Mei 4, 2023  ameendelea na zoezi la utatuzi  wa Kero za  papo kwa hapo Katika Wilaya ya Ikungi kata ya Sepuka Kijiji Cha Mnang'ana  kilichopo Wilaya ya Ikungi Mkoani Singida ambapo  Kero 52 zilisikilizwa na kupatiwa ufumbuzi .

Akiwa Kijijini hapo RC Serukamba  akipokea Kero za ukosefu wa maji, Barabara, migogoro ya ardhi na uharibifu wa maziringira ambapo alitoa maagizo kwa menaja wa RUWASA, TARURA na watendaji wa Serikali za vijijini na  kwenda kutatua Kero hizo.

Aidha RC amewaagiza wakandarasi wanaokarabati au kutengeneza Barabara kuhakikisha hawakati miti pasipokuwa na Sababu kwa kuwa Mkoa upo Katika utekelezaji wa kampeni ya kupanda miti na utunzaji wa Mazingira ikiwa ni maelezo baada kuwasilishwa kwa Kero ya ukataji miti ambayo haipo kwenye Barabara 

Hata hivyo Serukamba amewataka viongozi wa Serikali kwenye kata na vijiji wahakikishe wanawasikiliza wananchi na kutatua kero zao badala ya kukaa ofsini huku akiendelea kuonya tabia za watu unaowanyanyasa wanawake kwa kuwanyima haki ya kumiliki ardhi.

Aidha, ameonya tabia za wafugaji kuchunga kwenye mashamba ya watu huku akizitaka kamati za vijiji kuangalia Mabwawa ya kunyweshea maji na kuweka Mkakati ya mifugo kutopita kwenye mashamba ya wakulima ikiwa ni pamoja na kulinda vyanzo vya maji kwa kupanda miti.


Share:

0 comments:

Post a Comment

Copyright © WAZO HURU | Powered by Blogger Design by ronangelo | Blogger Theme by NewBloggerThemes.com