METDO Tanzania

METDO Tanzania

Thursday, March 9, 2023

SHIRIKA LA TYVA LAWAKINGIA KIFUA VIJANA

Na Saida Issa,Dodoma

Katika kuelekea bajeti ya mwaka wa fedha 2023/24 Shirika lisilo la Kiserikali la Vijana kupitia mradi wa vijana makini (TYVA) limeiomba Serikali katika mikopo inayotolewa na Halmashauri kwaajili ya Vijana iongezwe asilimia nne ili kuwasaidia kuweza kujikwamuwa kiuchumi .


Akizungumza Jijini Dodoma Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la vijana kupitia mradi wa vijana makini (TYVA) Yusuph Bwango alisema Serikali inapaswa kusimamia maeneo ya uwezeshaji wa kifedha na mikopo yenye masharti nafuu lengo  kuwainua vijana kiuchumi kupitia mikopo ya Halmashauri.


"Tunatambua serikali imefanya kazi kubwa sana kuhakikisha kwamba mikopo ya halmashauri ya asilimia 4 inaenda kwa vijana kwa wingi lakini vijana walitamani  kuona ile mikopo ikiongezeka na masharti yake yawezekuwa nafuu zaidi kuweza kuwafanya vijana waweze kujikwamua kiuchumi na kuendesha shughuli zao za kijasiliamari na kiuchumi kwa upana,"alisema.

Pia alisema kuwa vijana wameguswa na tozo zilizowekwa na Wizara ya fedha kwa kupitia sheria ya fedha na kwamba vijana wameomba kupitia bajeti ya mwaka 2023/24 serikali iweke tozo himilifu Kwa vijana na kuangalia sekta zingine ambapo Serikali itaweza kukusanya fedha kwaajili ya kufidia bajeti ya serikali.

"Katika tafiti tumeweza kuona Serikali kwa Mwaka inakadiriwa kupoteza zaidi ya Dola bilin 7.6 ulichukua asilimia 20 ya fedha ambayo Serikali inapoteza kupitia michakato mbalimbali ya kikodi inaweza ikalipa zaidi ya walimu laki moja na themanini Nchi nzima wa shule za msingi na awali,

"serikali inaweza ikajenga Madarasa zaidi ya 200,000 Nchi nzima kama zikitumika zile fedha ambazo zinapotea kwaiyo vijana wanaona Serikali kunahaja ya kuongeza nguvu kwenye maeneo ambayo inapoteza hela kwa wingi na kupunguza maeneo ambayo vijana wanaumia sababu maeneo hayo yakikusanya fedha kwa wingi vibaumbele vya vijana vitatatuliwa pamoja na changamoto zao,"alisema.

Naye Fred Mtei mtetezi wa vijana kutoka taasisi ya maendeleo ya vijana alisema kuwa kutokana na uchambuzi walioufanya uliwalenga vijana sababu vijana ni asilimia 34.5 inayokadiriwa kuwa asilimia 35 na wanachangia nguvu kazi ya Taifa asilimia kwa asilimia 64.5 na kuwa nikundi kubwa katika Taifa Kwa mujibu wa takwimu za NBs.

Alisema kuwa vijana ndio kundi kubwa linalochangia katika nguvu kazi ya Taifa na ukizungumzia Taifa huwezi acha zungumzia kundi la vijana ndio sababu wamejikita katika kundi hilo.

"Nitatumia takwimu za nyuma kabla ya sasa hivi sababu hazijatoka takwimu za nyuma za 2012 za NBs zinaonesha kwamba vijana ni asilimia 34.5 ambazo zinakadiriwa kuwa asilimia 35 kwamba wanachangia nguvu kazi ya Taifa asilimia 64.5 kwaiyo nikundi kubwa kwa Taifa letu,"alisema Mtei.

Kwa upande wake Dkt.Thea Mtala mbunge muwakilishi wa vyuo vikuu alisema kuwa Kutokana na kuwepo kwa tatizo la utafiti ni muhimu Serikali ikabuni kuweza kupata vijana katika kila Wizara au sekta ambao watakuwa wanafanya tafiti kwa urahisi na wepesi na kupeleka majibu katika Serikali ili iweze kuona namna ya kufanya ufumbuzi katika tafiti hizo.

Alisema kuwa kumekuwa na tamaduni ya kuziachia Wizara zifanye tafiti zenyewe kitendo kinachopelekea tafiti nyingi kutopata ufumbuzi.

"Nivizuri pia Serikali ikabuni kupata vijana katika kila wizara au katika kila sekta ambao watakuwa wanaweza kufanya tafiti zetu kwa urahisi na wepesi na kupeleka majibu katika Serikali ili Serikali iweze kuona namna gani sasa itafanya ufumbuzi katika eneo hilo la utafiti hasa kama utafiti huo tayari umetoa mapendekezo yakapelekwa katika kila wizara itakuwa ni rahisi

Suala la kuziachia Wizara zenyewe kufanya tafiti zinachukuwa muda mrefu lakini tukiwa na kundi la vijana wao kazi yao ikawa ni kufanya tafiti lakini pia inakuwa ni ajira kwao,"alisema
Share:

0 comments:

Post a Comment

Copyright © WAZO HURU | Powered by Blogger Design by ronangelo | Blogger Theme by NewBloggerThemes.com