METDO Tanzania

METDO Tanzania

Thursday, March 9, 2023

JWTZ YATANGAZA NAFASI ZA KUJIUNGA KWA VIJANA

Na Saida Issa, Dodoma

Jeshi la ulinzi la wananchi Tanzania(JWTZ) limetangaza nafasi za kujiunga na jeshi kwa vijana wa kitanzania wenye elimu ya kuanzia kidaato cha nne hadi shahada ya uzamili ambao wamemaliza mkataba  wa miaka miwili wa mafunzo ya kujitolea  katika jeshi la kujenga taifa na kurudishwa majumbani.

Akitoa taarifa hiyo kwa waandishi wa Habari leo march 9 2023 Jijini Dodoma kaimu mkurugenzi wa Habari   na uhusiao wa JWTZ, Luteni Kanali GAUDENTIUS ILONDA, amesema nafasi hizo zinawahusu  vijana wenye umri kuanzia miaka 18 hadi 26 kwa  wenye elimu ya kidato cha 4 na cha sita na umri usiozidi miaka 27 kwa wenye elimu ya juu.

Aidha,Luteni Kanali ILONDA, ameeleza vigezo vitakavyozingatiwa wakati wa katika maombi hayo kuwa mwombaji awe raia wa  Tanzania wa kuzaliwa mwenye kitambulisho cha Taifa,awe na afya nzuri na akili timamu,awe na cheti halisi cha kuzaliwa,vyeti vya shule nav yeti vya taaluma.

Vigezo vingine ni pamojana na awe hajatumikia Jeshi la Polisi,magereza,Chuo cha Mafunzo au Kikosi maalumu cha kuzuia magendo na asiwe ameoa au kuolewa.

Sambamba na Hayo amewataka wananchi kutorubuniwa na Matapeli bali jeshi la wananchi halijuani na mtu yoyote yule.

Kwa upande wa utaratibu wa jinsi ya kutuma maombi Luteni Kanali Ilonda ,amebainisha kuwa maombi yote yaandikwe kwa mkono na yawasilishwe makao makuu ya jeshi hilo Dodoma kwanzia leo tarehe 9,Machi hadi tarehe 20 ,Machi 2023 yakiwa na viambatanisho kama vile nakala ya kitambulisho cha taifa au namba ya nida,nakala ya cheti cha kuzaliwa,vyeti vya shule na chuo,nakala cheti cha JKT nan amba ya simu ya mkononi ya muombaji.
Share:

0 comments:

Post a Comment

Copyright © WAZO HURU | Powered by Blogger Design by ronangelo | Blogger Theme by NewBloggerThemes.com