METDO Tanzania

METDO Tanzania

Monday, February 13, 2023

WAZIRI MKENDA APIGA MARUFUKU VITABU 16 KUTUMIKA MASHULENI

Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Mhe.Prof Adolf Mkenda amepiga marufuku vitabu 16 kutumika mashuleni kutokana na vitabu hivyo kukinzana na mila,desturi na tamaduni za kitanzania .

Akizungumza na waandishi wa habari leo Februari 13,2023 jijini Dodoma kuhusu kufutwa kwa vitabu hivyo,Prof.Mkenda amesema, uwepo wa vitabu hivyo pia unahatarisha malezi bora ya watoto na kwa shule ambayo itabainika kuendelea kutumia vitabu hivyo mara baada ya katazo la Serikali itachukuliwa hatua mbalimbali za kinidhamu na kisheria ikiwemo kufutiwa usajili wake.

Amevitaja vitabu vilivyopigwa marufuku kutumika mashuleni ni pamoja na Diary of Wimpy Kid,Dairy of Wimpy Kid-Rodrick Rules,Diary of Wimpy Kid- The last Straw,Diary ofi Wimpy Kid –The Ugly Truth na Diary of Wimpy Kid-Cabn Fever.

Vitabu vingine vilivyopigwa marufuku hiyo ni Diary of Wimpy Kid –The Third Wheel,Diary of Wimpy Kid –Hard Luck,Diary of Wimpy Kid-The long Haul,Diary of Wimpy Kid –Old SchoolDiary of Wimpy Kid-Double Down na Diary of Wimpy Kid-The Gateway.
Share:

0 comments:

Post a Comment

Copyright © WAZO HURU | Powered by Blogger Design by ronangelo | Blogger Theme by NewBloggerThemes.com