METDO Tanzania

METDO Tanzania

Tuesday, February 14, 2023

CCM TUTAJIBU HOJA KWA VITENDO NA USHAWISHI-DKT SOPHIA MJEMA

Na Mathjas Canal, Shinyanga

Katibu wa Siasa na Uenezi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Taifa Dkt Sophia Mjema jana tarehe 14 Februari 2023 amewasilia mkoani Shinyanga.

Akizungumza na Viongozi mbalimbali wa chama hicho ngazi ya mkoa na Wilaya amesisitiza kuwa hakuna chama chochote kitakachoisumbua CCM katika uchaguzi wa serikali za mitaa na uchaguzi mkuu.

Amesema kuwa CCM itaendelea kuchaguliwa na wananchi kutokana na weledi wa kazi inazozifanya kupitia serikali yake inayoongozwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Dkt Samia Suluhu Hassan

Dkt Mjema amesema kuwa viongozi wa Chama Cha Mapinduzi wana wajibu wa kujibu hoja mbalimbali kwa vitendo na ushahidi kamili kwani kufanya hivyo itaondoa majungu.

Amesisitiza kuwa viongozi hao wana wajibu wa kufanya kazi ya kutangaza sera za CCM na Ilani yake hivyo kupitia mikutano mbalimbali ya kuimarisha chama wanapaswa kueleza mafanikio ya serikali.

Kadhalika, Dkt Mjema ameupongeza uongozi wa CCM mkoa wa Shinyanga kwa kusimamia kwa umakini mkubwa maadhimisho ya miaka 46 ya chama hicho kwani maadhimisho hayo yamekuwa na mafanikio makubwa.

MWISHO
Share:

0 comments:

Post a Comment

Copyright © WAZO HURU | Powered by Blogger Design by ronangelo | Blogger Theme by NewBloggerThemes.com