METDO Tanzania

METDO Tanzania

Thursday, February 9, 2023

MAMLAKA YA KUSIMAMIA UVUVI WA BAHARI KUU KUJENGA KIWANDA CHA KUCHAKATA SAMAKI



Na Rahma Hajia,Getrude Vangayena Dodoma.

Mamlaka ya kusimamia uvuvi wa bahari kuu nchini  ina mpango wa kujenga kiwanda cha kuchakata samaki ambacho kitasaidia kuongeza ajira kwa watanzania pamoja na kuendela kusimamia na kuratibu shughuli za uvuvi katika bahari kuu.

Akizungumza na wanahabari  jijini Dodoma  Mkurugenzi mkuu wa mamlaka ya kusimamia uvuvi wa bahari kuu Dkt. Emmanuel Sweke amewataka wavuvi   kulinda mazingira ya bahari kwa kuacha matumizi ya uvuvi haramu.

Aidha Katika hatua nyingine Dkt.  Sweke amesema gharama za leseni kwa wavuvi wa ndani ya nchi ni nafuu tofauti na wavuvi wa  nje ya nchi katika bahari kuu ili kuhamasisha watanzania kuchangamkia fursa za uvuvi katika bahari kuu.

‘’Mamlaka ya kusimamia uvuvi wa bahari kuu ndio mamlaka inayohusika  na utoaji wa leseni  ya uvuvi katika pande zote mbili ambazo ni Tanzania  bara pamoja visiwani’’.

‘’Pia Taasisi hii inajishughulisha na kuratibu  shughuli zote za uvuvi katika bahari ambapo makao makuu ya taasisi hiyo yapo Zanzibar,’’amesema sweke.

Hata hivyo alimalizia kwa kusema kuwa pindi kiwanda cha kuchakata samaki   kitakapojengwa mkoani Tanga kitakuwa na uwezo wa kuchakata tani mia moja hadi mia mbili za samaki kwa siku ambapo kiwanda  hicho kitaweza kutoa ajira kwa watanzania mia moja.  

Mamlaka ya kusimamia uvuvi wa bahari kuu ni Taasisi ya muungano yenye jukumu la kusimamia na kuratibu shughuli zinazohusiana na uvuvi wa bahari kuu ikiwemo utoaji wa leseni za uvuvi pamoja na kuhakikisha mazingira ya bahari yanalindwa vizuri.                      

Share:

0 comments:

Post a Comment

Copyright © WAZO HURU | Powered by Blogger Design by ronangelo | Blogger Theme by NewBloggerThemes.com