Na Saida Issa Dodoma.
MAMLAKA ya Mapato Tanzania (TRA)imenza kuwafikisha Mahakamani watuhumiwa mbalimbali katika Mahakama ya Wilaya ya Mkoani Dodoma akiwemo Agness Victor mwenye umri wa Miaka 46Mkazi wa Ilazo Jijini Dodoma ambaye alinunua Vitenge na kanga bila kudai risiti pamoja na kukataa kumtaja aliyemuuzia bidhaa hizo.
Akimsomea Shitaka hilo miongoni mwa washitakiwa hao,mbele ya Hakimu Mwandamizi wa Mahakama hiyo,Nyambuli Tungaraja ,Jijini Dodoma Mwanasheria wa Mamlaka ya Mapato Mkoa wa Kikodi Dodoma Hadija Senzia amesema mama huyo anashitakiwa Kwa mujibu wa Kifungu Cha 86 kifungu kidogo Cha nne Cha sheria ya usimamizi wa kodi namba kumi ya Mwaka 2015 ya kushindwa kudai risiti ya Kielektroniki.
Wakili huyo ameeleza kuwa mshitakiwa huyo anadaiwa kutenda kosa hilo mnamo Mwaka huu katika eneo la barabara ya nane wakati Maafisa wa TRA wakitekeleza majukumu yao ya kikazi na kufanikiwa kumkamata akiwa na mzigo wa vitenge kadhaa akiwa hana risiti za kielekttoniki.
Mwanasheria huyo amesema kuwa kuhusu kosa la pili la Mshitakiwa kutotoa ushirikiano ni kwa mujibu wa kifungu 85, kifungu kidogo 3 (h) cha sheria ya Utawala wa Kodi na Usimamizi wa Kodi namba 10 ya mwaka 2015
Kwa Upande wa Hakimu alipomuuliza Mtuhumiwa Agness kuhusiana na kutenda kosa hilo mshitakiwa Agness alikana Shitaka hilo la pili na kukubali Shitaka la kwanza la kutodai risiti.
Hata hivyo Hakimu Tungaraja ameahirisha Shauri hilo la Jinai namba 171 la Mwaka 2022 ambalo litatajwa tena Januari 3 Mwaka 2023.
Mshitakiwa Agness amekidhi Masharti ya Dhamana hadi shauri litakapo tajwa tena .
0 comments:
Post a Comment