Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi Abdallah
Ulega ,akizungumza wakati wa kufungua soko la samaki la Nyakaliro
lililopo Halmashauri ya Buchosa Mkoani Mwanza.
Hili ndiyo jengo la soko la Nyakalilo lililofunguliwa na Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe.Abdallah Ulega
………………….
Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi Abdallah
Ulega amefungua soko la samaki la Nyakaliro lililopo Halmashauri ya
Buchosa Mkoani Mwanza.
Soko hilo lililokuwa limefungwa miaka
mitatu iliyopita kutokana na kutokuwa na usimamizi mzuri ikiwemo
uzalishaji mdogo wa samaki na dagaa pamoja na mianya ya utoroshaji wa
mazao ya uvuvi.
Ulega alisema, Rais amewatengenezea miundombinu ya soko kwa maslahi mapana ya taifa kwa kutaka wananchi wafanye kazi.
“Sasa tumeisha weka mfumo mzuri wa
usimamizi ndio maana leo tumefungua soko hili, ili mapato ya Serikali
yaweze kukusanywa kwa haki na wananchi wa maeneo haya waweze kufanya
shughuli za kujiingizia kipato,” alisema Ulega.
Hivyo alimuagiza,Mkurugenzi wa
Halmashauri ya Buchosa Crispin Luanda, kufanyia maboresho haraka soko
hilo hili wananchi waanze kufanyabiashara huku akisisitiza kuwa
mfanyabiashara akiwa amekata vibali kutoka eneo moja anaruhusiwa kufanya
biashara sehemu yoyote bila kubuguziwa na jambo hilo atalisimamia.
Pia aliutaka uongozi wa uvuvi Kanda ya
Ziwa leo( jumatatu) kumpeleka ofisa ambaye atakuwa anasimamia ukaguzi na
kutoa vibali katika soko hilo,pamoja na DED Buchosa kutafuta mawakala
wa huduma za kifedha sokoni hapo ili kuwapa urahisi wafanyabiashara.
Aidha alitumia fursa hiyo kwa kusema,
ataka na wataalamu wa uvuvi ili kupitia na kuangalia sheria inayokataza
samaki ambaye ajachakatwa kuuzwa nje ya nchi kwa maslahi mapana ya
taifa.
Ili waweze kuruhusu ata wale ambao
hawawezi kuuza viwandani kufanyabiashara, hivyo kwa kufanya utafiti na
kuona kama samaki akiuzwa nje bila kuchakatwa mvuvi atapata mapato na
taifa pia.
Kwa upande wake Mkuu wa Idara ya Mifugo
na Uvuvi Halmashauri ya Buchosa Shija Lyella alisema,wananchi
wanashukuru kwa kufunguliwa soko hill la Nyakaliro ambalo ni chanzo
muhimu cha mapato ya halmashauri hiyo na kichocheo cha uchumi kwa wadau
wa sekta ya uvuvi ndani na nje.
“Lengo ni kutoa huduma ya soko kwa wadau
Wa uvuvi wa dagaa na samaki wakavu,kuiwezesha halmashauri kukusanya
mapato yatokanayo na ushuru wa mazao ya uvuvi,kuchochea Biashara ndogo
ndogo pamoja na kutoa ajira kwa wananchi Wa maeneo husika.Kijiografia
soko hili lina nafasi kubwa zaidi ya kuwa la kimataifa kwa sababu za
uzalishaji wa mazao ya uvuvi unaokadiriwa kuwa tani 4000 za dagaa na
2600 za samaki kwa mwaka,”alisema Lyella.
Naye Mbunge wa Jimbo la Buchosa
Dkt.Charles Tizeba alimuomba, Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi Abdallah
Ulega aiagize Halmashauri ya Chato kuacha kuwasumbua wafanyabiashara
wanaonunua samaki kutoka katika soko la Nyakaliro pamoja na kuruhusu
uuzwaji wa samaki nje ambao hawajachakatwa.
0 comments:
Post a Comment