METDO Tanzania

METDO Tanzania

Wednesday, December 14, 2022

IKUNGI NA UJENZI WA VYUMBA VIPYA 29 VYA MADARASA

 












Mkuu wa wilaya ya Ikungi Mheshimiwa Jerry C. Muro leo tarehe 14/12/2022 amefanya ziara ya ukaguzi na kupokea taarifa ya ujenzi wa vyumba vipya vya madarasa 29 katika shule 16 za majimbo ya singida mashariki na singida magharibi ujenzi ambao umegharimu shilingi milioni 580

Mhe. Muro akiwa pamoja na mhandisi wa halmashauri Millinga na afisa elimu sekondari Mwalimu Ngwano wametembelea shule zote 16 na kujiridhisha na kazi inayoendelea ya ujenzi ambapo mpaka kufikia leo ujenzi umeshakamilika kwa asilimia 99

Katika ziara hiyo Mhe. Muro pia amejionea zoezi la uwekaji wa viti na meza katika kila darasa kazi ambayo inaendelea kwa madarasa yote 29 na kusisitiza zoezi lazima liwe limekamilika mpaka kesho asubuhi tayari kwa ajili ya makabidhiano kwa Mkuu wa mkoa wa Singida Mheshimiwa Peter Serukamba siku ya alhamisi tarehe 15/12/2022

Share:

0 comments:

Post a Comment

Copyright © WAZO HURU | Powered by Blogger Design by ronangelo | Blogger Theme by NewBloggerThemes.com