METDO Tanzania

METDO Tanzania

Saturday, September 10, 2022

WAZIRI MKENDA AFANYA MAZUNGUMZO NA BALOZI WA IRAN NA MKUU WA CHUO CHA KIMATAIFA CHA JAMIAT


Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Mhe Prof. Adolf Mkenda (Mb) juzi amekutana na kufanya mazungumzo na Balozi wa Iran nchini Tanzania Mhe Alvandi Hossein pamoja na Mkuu wa Chuo Kikuu cha Kimataifa cha Jamiat - Mustafa Al Alamiya cha nchini Iran Dkt Ali Abbasi.

Katika mazungumzo hayo Waziri Mkenda na wageni hao kutoka Iran, wamekubaliana kuendeleza ushirikiano kwenye Taasisi za elimu ya Juu katika maswala ya Teknolojia, Sayansi, na Elimu ujuzi.

Waziri Mkenda amemwomba Balozi huyo kutoa ufadhili wa masomo kwa wanafunzi wa elimu ya juu na kubadilishana utaalamu baina ya Vyuo Vikuu vya hapa nchini na Iran ili kuongeza wigo wa ujuzi kwa pande zote mbili.

Kadhalika, Waziri Mkenda amemueleza Balozi huyo wa Iran kuwa Tanzania inafanya mapitio ya Sera ya Elimu na Mafunzo ya Mwaka 2014 na mabadiliko ya mitaala ili kuongeza ubora wa elimu na mafunzo.

MWISHO
Share:

0 comments:

Post a Comment

Copyright © WAZO HURU | Powered by Blogger Design by ronangelo | Blogger Theme by NewBloggerThemes.com