METDO Tanzania

METDO Tanzania

Tuesday, August 23, 2022

UWT MISUNGWI YAKABIDHIWA MIZINGA YA NYUKI 50 KUKUZA MRADI WA UFUGAJI NYUKI






Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe.Mary Masanja (Mb) amekabidhi mizinga ya nyuki 50 kwa Jumuiya ya Wanawake Tanzania (UWT) ya Wilaya ya Misungwi kwa ajili ya kuendeleza mradi wa ufugaji nyuki.

Akizungumza leo katika Ofisi za UWT Misungwi Mhe. Masanja amesema mizinga hiyo imegharimu kiasi cha shilingi milioni tano.

“Naahidi kuongeza mizinga mingine endapo itaendelea kuleta faida kwa jumuiya” Mhe. Masanja amesisitiza.

Amefafanua kuwa mradi huo wa ufugaji nyuki utasaidia mapato ya jumuiya kutokana na mazao ya nyuki ambayo ni asali, nta na sumu ya nyuki ambayo soko lake ni la uhakika.

Mhe. Masanja amefafanua kuwa kupitia mapato yanayotokana na miradi ya jumuiya, itaiwezesha kujisimamia yenyewe hasa katika kukidhi mahitaji muhimu ya wanajumuiya.

Aidha, amewapongeza viongozi wa UWT Misungwi kwa kusimamia vizuri miradi ambapo wameweza kuzalisha lita 40 za nyuki zenye thamani ya shilingi laki nne kutokana na mizinga ya nyuki mitano ya awali.

Pia, Mhe. Masanja ameahidi kuipatia jumuiya hiyo pikipiki  nyingine kwa ajili ya kuendeleza mradi wa pikipiki.

Naye, Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Misungwi , Cholage Mohamed Cholage amewataka viongozi wa UWT Misungwi kuwa waaminifu kwenye kusimamia miradi ya jumuiya ili ilete manufaa yalikosudiwa.

Pia, amempongeza na kumshukuru Naibu Waziri Masanja kwa kuwa na moyo wa kuijitolea mizinga 50 kwa jumuiya ya UWT Misungwi.

Naibu Waziri Masanja anaendelea na ziara katika Kanda ya Ziwa ikiwa ni utekelezaji wa majukumu yake ya kila siku

Share:

0 comments:

Post a Comment

Copyright © WAZO HURU | Powered by Blogger Design by ronangelo | Blogger Theme by NewBloggerThemes.com